Mwakyembe acha kutudanganya...usanii sasa basi ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwakyembe acha kutudanganya...usanii sasa basi !

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Dec 2, 2009.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Dec 2, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280

  Wote wamesimama kwenye mvua, moja atishia kumlowesha mwenziye !
  Wote wanaogelea kwenye tope, moja adai aliyechafuka labda mwenziye !
  Wote wamtumikia bwana moja, hakuna wa kumsaliti mwenziye !
  Kwani
  Wote huunganisha nguvu, anapotokea mpinzani.
  Hili la Mwakyembe hakika ni changa la macho, jamani angalieni
  Hakuweza kuyasema bungeni ama NEC, sasa ataka kuyaanika uchochoroni !
  Lakini
  Si wadanganyika wapo na watachangamkia tenda ?
  Wanachosahau ni kuwa toka lini mafahali wawili wakakaa zizi moja ?
  Linapotokea hivyo ama moja kishashikishwa adabu, vipi awike tena ?
  Hata hivyo
  Kila kivumacho kina mwisho, historia haina tabia ya uwongo.
  Kama limetokea limetokea, kudai vinginevyo ni kujaribu kupindisha ukweli
  Waliapa kuwa watalindana, sasa huu usanii ni wa nini ?
  Ni uwongo
  Wananchi wengine tumeamka zamani na hivi sasa tuko macho.
  Ili ziweze kupigwa kavu kavu ni bidi watokee kona tofauti ulingoni.
  Moja akivaa mkanda mwekundu na mwenziye akivaa mkanda wa bluu.
  Huo ndio utaitwa mpambano.
   
 2. Mambo Jambo

  Mambo Jambo JF-Expert Member

  #2
  Dec 2, 2009
  Joined: Jul 11, 2008
  Messages: 1,100
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Haya maneno ulikuwa unamaanisha kama yalivyo au ulikuwa unababatiza ili vina na beti zikae sawa?..
   
 3. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #3
  Dec 2, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Wewe umesema.
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Dec 3, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,578
  Likes Received: 3,876
  Trophy Points: 280
  You are right Magi3,

  watu wakiambiwa hivi huwa wanatoka povu la hasira.Kichama RA anacheo zaidi ya Mwakyembe, ili Mwakyembe huyu awe mbunge atapitishwa na CCM ambayo kwayo kuna mafisadi, kumbuka mafisadi CCM sio RA tu kama Mwakyembe anavyotaka kufunika funika na kutaka tuamini hivyo.CCM mafisadi ni wote , katika hao mwakyembe yumo mzimamzima!

  CCM ni dampo, Mwakyembe kama msafi hawezi akaishi dampo, vile vifedha fedha vya ubunge vilivyomfanya akimbie kufundisha UDSM ni vitamu! na atataka kuendelea kuvila, na ili iwe hivyo lazima apate baraka za viongozi wa CCM ambao ni mafisadi!

  Mwakyembe ameishawateka wengi humu , huwezi kuamini ukianza kiuwataja majina utalia!

  alishafanya kazi ya Richmond, kama serikali haichukui hatua, akajiuzulu kuonyesha kutounga mkono serikali ya chama chake! hapo anakuwa mpiganaji haswaaa!
   
 5. Malafyale

  Malafyale JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 11,209
  Likes Received: 3,622
  Trophy Points: 280

  Nimesoma tena na tena hii habari yake lkn bado sijajua alikuwa anataka kuongea nini,kwa ufupi habari yake haieleweki na ipo irrelevant na kichwa cha habari chenyewe,ni upupu mwingine ndani ya JF yetu tukufu kwa kweli
   
 6. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Mwakyembe msanii tu..to me he is an opportunist hana lolote la maana
   
 7. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #7
  Dec 3, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Na kweli huelewi ndio maana unarusha matusi! Matusi ni dalili mojawapo ya kutoelewa!
   
 8. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #8
  Dec 3, 2009
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  Mwakyembe arudi akafundishe..haelewi anachofanya
   
 9. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #9
  Dec 3, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Heshima mbele Dr Mwakyembe.

  Heri lawama kuliko fedheha. Siasa ina wenyewe, rudi chuo kwenye kazi yako kulinda hishma yako.
   
 10. Mwana va Mutwa

  Mwana va Mutwa JF-Expert Member

  #10
  Dec 3, 2009
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 429
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  batoto ba kyela bameamka bana
   
 11. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #11
  Dec 3, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Penye mtama mwingi, mwaga kuku - watadonoana lakini wana hakika ya kushiba, funguo za ghala si zipo ? Ndugu wawili hugombana lakini jioni huketi meza moja kwa chakula - ole wako utake kuwapokonya huo mlo, utajuta. Mkuu wa kaya hutoka na kuwaacha wanawe tisa nyumbani, kumtafuta wa kumi aliyepotea na anapompata humkanya kwa tabia yake. Mwakyembe analilia mdahalo kwenye luninga ili aweze kupita Kariakoo akiwauliza machinga ambao wameshindia mhogo mchana kutwa nani zaidi, yeye ama RA. Anajua wazi kuwa kura zikipigwa ndani ya NEC hafui dafu, si walionja joto la jiwe walipodhani na wao wamekomaa na wana ubavu. Anajua wazi CCM iko mikononi mwa nani lakini yeye naye si amejibanza humo humo ndani ya nyumba ya wenyewe ? Sasa mdahalo wa nini na kwa faida ya nani, sana sana tototundu litacharazwa viboko na kuonywa lisirudie - mambo kwisha, kaput. Anatafuta manukato mitaani na usiku anarudi kulala kwenye nyumba ile ile na kujifunika shuka lile lile lenye uvundo - masikini Mwakyembe. Hapana Dr. usiendelee kutudanganya, huo usanii sasa basi !
   
Loading...