Mwakilishi wa Kundi la wanavyuo kaongea point

Mwakilishi wa Kundi la wanavyuo kaongea point

Eng. Y. Bihagaze

JF-Expert Member
Joined
Sep 8, 2011
Posts
1,487
Reaction score
913
Jioni hii wakati nasikiliza Bunge hili tata la Katiba kuna bidada mmoja amesema kitu makini sana, amesema Yeye Ni mwakilishi wa Kundi la wanavyuo, alichosema nadhani amefunga mjadala wa Kura ya SIRI AMA UWAZI.. Kama Bunge Lina watu wenye vichwa sio mazezeta nadhani wathamini Hoja ya bidada huyu 22years old Na mjadala Ufungwe... Kasema..

Yeye Kama mwakilishi wa Kundi kubwa la wanachuo Na kizalendo asingependa kulivuruga Kundi lake, ambalo miongoni mwao kuna wenye mtazamo wa Kura IWe ya Wazi wengine IWe ya Siri Kwenye maamuzi mbalimbali ya Kimjadala Bungeni. Endapo atapiga Kura ya wazi Na kuegemea upande mmoja wa hoja ni wazi atajiletea mtafaruku Kwa wajumbe wa Kundi lake wenye mtazamo tofauti na yeye lazima kuwe Na kutoelewana baada ya Bunge hili.

Ni wazi pia Kwamba HATA Wabunge/wajumbe wanaopendekeza Kura IWe ya wazi sidhani Kama waliowatuma wote wana mtazamo Sawa Na Yeye. Mfano Askofu mkuu Mtetemela Na Kundi kubwa la maaskofu wa CCT sidhani Kama maaskofu wote watakubaliana Kwenye Hoja moja hivyo akipiga Kura ya wazi Basi atakuwa amejitengenezea pengo La uadui Na ugomvi Ndani ya kundi lake.

Mie nadhani baadhi ya wabunge wamelewa uelewa Kwamba Kama Wewe ni Mbunge wa Jimbo flan Kwa TIketi ya CHAMA flani, WEWE si Mbunge wa jimbo Hilo Kwa wananchi wa CHAMA chako tu Bali ni Mbunge wa wananchi wote wa jimbo Lako Kwa vyama Na makabila Yao, Na baada ya uchaguzi umeibuka mshindi huendi kuwawakilisha wananchi wa chama chako pumbav wewe unakwenda kuwawakilisha wananchi wote wa jimbo Lako. Ni Ulevi Na uchizi kuamini kwamba Eti Kura yako ya wazi Kwenye maamuzi yako ndivyo ulivyotumwa Na wananchi wote wa Jimbo Lako.
 
Mkuu hata mimi nilifuatilia hoja za yule dada nikashawishika kumuunga mkono na kama wabunge wote wana akili timamu basi huyu dada kafunga mjadala ila hawakosi wa kupinga na wanaruhusiwa.
 
Eng. Y. Bihagaze, kura ya wazi kwenye masuala nyeti, kama muundo wa Muungano, ni UZEZETA!!!!! Haukubaliki!!!!! MiCCM inataka kuturudisha zama za Old Stone Age!!!! Eti tuwe wa kwanza duniani kuwa na aina mbili za kura, ya siri na ya wazi, katika suala moja!!!! AIBU HII HAIVUMILIKI!!! Tutajificha wapi Watanzania, katika macho ya Jumuia ya Kimataifa?????????
 
Huu mchakato una mambo! Sijui kama katiba mpya ya wananchi itapatikana, nasema labda lakini sina uhakika.
 
Kama bidada anawakilisha kundi kubwa la wasomi ambalo nalo limegawanyika pande mbili kuu za usiri na uwazi kwa nini hawakupiga kura kwa minajiri ya kuja na msimamo wa kundi la wasomi.
Kimsingi kura ya wazi ndiyo inawafaa watu wasaliti kama huyu. Wenzake wamemtuma nin: Wengi awape haki yao.
 
Huyu bidada mnayemsifia amejichanganya, wafuasi wake wamemtuma kwenda kuzingatia masilahi ya kundi lake ktk katiba, katiba sio kura ya wazi au ya siri wala mambo hayo hawakuyajua, wanafunzi wanamitazamo yao ktk vipengere mbalimbali ndani ya rasimu ndiyo kazi waliyomtuma, hayo makundi mawili anaongea unafiki!!
 
Kama bidada anawakilisha kundi kubwa la wasomi ambalo nalo limegawanyika pande mbili kuu za usiri na uwazi kwa nini hawakupiga kura kwa minajiri ya kuja na msimamo wa kundi la wasomi.
Kimsingi kura ya wazi ndiyo inawafaa watu wasaliti kama huyu. Wenzake wamemtuma nin: Wengi awape haki yao.

Halikadhalika Kama Wewe Ni Mbunge Rudi Kwa watu wa jimbo Lako zaidi ya Laki mbili waulize mmoja mmoja wanataka Nini ndipo upeleke uwakilishi wako Kama utaweza.. Watu wengine wanaongea wasichokijua
 
Ulisikia lakini kijembe kwamba HAOLEWI HUYOOOO! Mazezeta huwezi kuwakwepa kila mahali
 
Kama bidada anawakilisha kundi kubwa la wasomi ambalo nalo limegawanyika pande mbili kuu za usiri na uwazi kwa nini hawakupiga kura kwa minajiri ya kuja na msimamo wa kundi la wasomi.
Kimsingi kura ya wazi ndiyo inawafaa watu wasaliti kama huyu. Wenzake wamemtuma nin: Wengi awape haki yao.

Wewe umemtuma nini mwakilishi wako?hapo bungeni watu wameenda kutafuta katiba mpya sii kutafuta wasaliti.Ungetumia nguvu hii pia kutaka mikataba inayoingia serikali iwe ya wazi ningekuona wa maana
 
Mtetemela kama mtoto mdogo nae kawagawa waumini wake,na kujipotezea heshima ili atukuzwe na hao viongozi wa CCM,bila soni kwa sauti kubwa alisema ndiooo,sijajua hao masheikh waliitika vipi kwani baada ya kumsikia baba askofu akigeuka mwanasiasa ilibidi nitoke niende grossary,sijui hawa watu watatumiwa mpaka lini,hata viongozi wa dini nao wanawagawa wananchi.
 
Hiyo ndo pointi?
Acha kutuwangia,
Me kama mmojawao niliyewakilishwa na huyo binti nataka nitambue alichoenda kukiwasilisha bungeni,na siyo kufanya vi2 kimyakimya.
 
Kipara cha baba askofu nilidhani kimefika hapo kwa sababu ya mafikara kumbe nae ni baba askofu wa politics Eti ndioooo yaani huko kanisani kwako hata shemasi tu anachaguliwa kwa kura ya siri leo hiii na wewe
 
Back
Top Bottom