Mwaka wa kwanza wa Intifadha ya Quds

Mwaka wa kwanza wa Intifadha ya Quds

Sinoni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2011
Posts
7,045
Reaction score
12,538
Mwaka wa kwanza wa Intifadha ya Quds
  • 4bhkd405f838c71nij_800C450.jpg
Leo tarehe Mosi Oktoba inasadifiana na siku ya kuadhimisha mwaka wa kwanza wa kuanza mapambano ya Intifadha ya Quds ya wananchi wa Palestina dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.

katika siku kama hii ya leo mwaka mmoja uliopita baada ya kushadidi mashambulizi ya walowezi wa Kiyahudi dhidi ya Msikiti wa al Aqsa na njama zao za kutaka kuugawa msikiti huo, wananchi wa Palestina walianzisha mapambano ya Intifadha ya Quds mbayo bado yanaendelea hadi hii leo. Takwimu za Kituo cha Utafiti cha Quds zinasema kuwa, Wapalestina 250 wameuawa shahidi kwa kupigwa risasi na askari wa Israel tangu kuanza kwa Intifadha ya Quds. Wapalestina wengine karibu elfu 18 na 300 wamejeruhiwa katika maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi na Quds huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu katika mapambano ya Intifadha ya Quds.

Duru mpya ya mapambano ya wananchi wa Palestina mbayo imepewa jila la Intifadha Mpya ya Quds au Intifadha ya Tatu ni tukio muhimu sana katika historia ya mapambano ya ukombozi ya Wapalestina dhidi ya maghasibu Wazayuni. Mapambano ya Intifadha ya Quds kama yalivyokuwa mapambano ya kabla yake, yamevuruga na kutibua njama na mahesabu ya utawala wa Kizayuni wa Israel za kutaka kutwaa maeneo zaidi ya Wapalestina hususan eneo la Quds tukufu. Utawala ghasibu wa Israel mbao ulikuwa katika ndoto kwamba, mwenendo wa eti mapatano ya Mashaiki ya Kati na usaliti wa baadhi ya nchi za Kiarabu dhidi ya malengo ya harakati za kupigania uhuru za Palestina vingeweza kuzima mwamko na harakati za wananchi wa Palestina, ulikabiliwa na wimbi kubwa la Intifadha ambalo limetikisa zaidi nguzo za utawala huo dhalimu kuliko ilivyokuwa huko nyuma.

4bhk6158722d481qgq_800C450.jpg

Intifadha ya Quds
Leo mapambano ya Intifadha ya Quds yamekamilisha mwaka mmoja huku askari wa utawala wa kikatili wakiendelea kuua raia wasio na hatia wa Palestina. Hata hivyo vijana shupavu na harakati za kupigania uhuru za Palestina kama Hamas na Jihad Islami zingali zinasisitiza na kutilia mkazo azma yao ya kudumisha mapambano hadi Quds tukufu na kibla cha kwanza cha Waislamu vitakapokombolewa kutoka kwenye makucha ya Wazayuni makatili.

Hapana shaka kuwa, Intifadha ya Quds na kushadidi kwake katika miezi ya hivi karibuni imeutia kiwewe zaidi utawala wa kigaidi wa Israel. Tangu baada ya nchi yao kuvamiwa na kukaliwa kwa mabavu na Wazayuni, Wapalestina daima wamekuwa wakitumia njia mbalimbali kuzima na kukwamisha sera na siasa za kifashisti za maghasibu hao licha ya kusalitiwa na nchi nyingi za Waislamu na Waarabu. Kuanza kwa mapambano ya Intifadha ya Kwanza hapo mwaka 2000 dhidi ya hatua za mara kwa mara za Wazayuni za kuuvunjia heshima Msikiti wa al Aqsa na kwa ajili ya kupinga hatua ya kichochezi ya waziri mkuu wa zamani wa Israel, Ariel Shaon ya kuingia katika eneo hilo tukufu ni kielelezo cha wazi cha azma kubwa ya Wapalestina ya kulinda ardhi na matukufu yao ya kidini.

Kwa kutilia maanani mafanikio hayo ya muqawama na mapambano, Wapalestina wanasisitiza kuwa, njia pekee ya kukomboa ardhi na maeneo yao ya matakatifu ni mapambano ya silaha. Hii ni kutokana na ukweli kwamba, Wazayuni maghasibu hawaelewi isipokuwa lugha ya mtutu wa bunduki.

4bk90efc141f5adxcv_800C450.jpg

Vikwazo dhidi ya Israel vinaongezeka
Miongoni mwa matunda ya mapambano ya Intifadha ya Quds ni kuwazindua walimwengu kuhusu masaibu yanayowapata wananchi wanaodhulumiwa wa Palestina. Vilevile Mapambano ya Intifadha yamezidisha vikwazo vya kimataifa dhidi ya utawala wa Kizayuni.

Ala kulli hal, mwenendo wa sasa unaonesha kuwa, mapambano ya ukombozi ya wananchi wa Palestina dhidi ya Wazayuni maghasibu hayajasimama bali hata yameingia awamu mpya na pana zaidi.

Cc:
 
Wakati unawaza vikwazo wenzio wamesain mkataba wa msaada wa kijesh wa miaka 10 na marekan
 
Back
Top Bottom