Mwaka Mpya; Fursa Mpya

freeboy

JF-Expert Member
Mar 24, 2011
242
191
Habari wanajamvi.

Nikiwa kama kijana niliyeamua kujiajiri mwenyewe kwa mtindo wa kipekee wa kuzifuata fursa.

Nimekuja jamvini ili nipate kujua RATIBA ZA MINADA HASA MAENEO YA PWANI kwa kuanzia ili nifanye utafiti wangu ni Biashara gani kwa kila mnada naweza peleka kwa wakati husika yenye soko ili kuweza kuandaa PLAN yangu ya MOBILE BUSINESS.

Nia na madhumuni yangu ni kua na ofisi inayotembea kwa kufanya biashara ktk minada hadi hapo nitakapoona sasa naweza kuwa na sehemu maalumu ya kufungua ofisi.

NB. Nimetaja maeneo ya PWANI kutokana na Mtaji nitakaoanza nao utaniwezesha kukidhi maeneo ya karibu hadi hapo mtaji utakapotanuka zaidi kwa maana naishi DAR.

Asante na Karibuni kwa ushauri zaidi nipate uzoefu wenu najua wengi tutajifunza hapa
 
mkuu wazo zuri saana. tabata kimanga upo huo mnada watu huwa wanakuja siku ya jnne kwenye barabara flani kabla ya kufika stand.

hao jamaa wanazunguka sehemu kibao.
 
Back
Top Bottom