What is so special about mwaka Mpya?
Tangu nikue na niwe na akili timamu nimeona shamrashamra nyingi kuhusu kupokea mwaka mpya kwa maana ya namba kuongezeka tangia nikiwa na akili timamu.
Enzi hizo nikiwa nimekulia katika nyumba za "kotazi" niliona mambo mengi hasa siku moja kabla ya "mwaka mpya"
Watu waliandaa mbuzi wa kuchoma wakati wakikesha kusubiria mwaka
Watu waliandaa madebe makubwa ya kugonga na kufurahia usiku huo
Wengine walienda ibada za mikesha usiku ili mwaka ukianza uwakute kanisani
Wengine walijipanga kukutana na wapenzi wapya
Wengine waliamua kubadili namna yao ya kuishi hasa katika mwaka unao anza
Vyote hivyo vilitendeka nikiwa naona na kwa namna moja ama nyingine niliweza kushiriki japo mambo mawili ama matatu katika umri ule
Kadiri muda unavyokwenda najiuliza "what is so special about mwaka mpya? "
Majibu mengi yananijia kichwani mwangu na labda naweza kuwa namtazamo tofauti kidogo na wengine!
"Na hii yaweza kuwa maana ya mwaka mpya"
Mwaka unapoanza yani kwa ongezeko la namba katika namba zile tutambue ni sisi wanadamu ndo tuliamua iwe hvyo, kwamaana hyo yaweza kuwa tofauti km tukiamua hvyo, mf mwaka utakapoanza tuuite jina lolote badala ya namba! ama tukaamua namba ziendelee ila ziwe zinapungua, ni maamuzi ya mwanadamu hayo na utashi alio kabidhiwa.
Wengi wamekuwa wakijiandaa kwa vyakula na vinywaji, binafsi naona nitofauti kidogo, vyakula na pombe ni vya kimwili tu na siyo ajabu vikaleta magomvi na kutokuelewana kwa wanafamilia ama ndugu.(hasa siku hyo ya mkesha)
Sikatazi kunywa na kula, nachomaanisha ni muhimu kwa mwanadamu wa leo kutambua kusudi Lake la kuwepo duniani.
Namshukuru Mungu kwa uwezo na nguvu alizonipa, nimekuwa nazitumia mara kwa mara japo bado sijafikia kiwango ambacho aliyenipa mamlaka ya kupumua "Mungu " kufikia, kila wakati kila dakika naomba huruma na utashi nitumie vyema uwezo na karama nilizojaliwa.
Watu wanywe Wale na washibe ila ni muhimu kutambua kusudi lako la kuwepo ukiwa unapumua, ni muhimu kutumia vyema kidogo ulichonacho ili uweze kutambua kusudi lako
Mwaka unapoanza, basi ni vyema siku kabla na baada ukafunga "mlo", "kinywaji" na kuwapatia wasiojiweza nawe utakuwa umefanya ibada tosha ya "utambuzi"
Jipime vyema je umetimiza kusudi la kupumua hadi leo? Jipime kwa kuangalia vitu mbali mbali
Je malengo yangu ya mwaka ulioisha yametimia? Km hapana rudi fanya ibada ya utambuzi
Km ndiyo yamefikiwa rudi fanya ibada ya utambuzi itakuonesha kusudi jipya la uwepo wako leo
Nakuambia mpendwa hata km ww siyo mkrisro/muislamu ,lazima unajua nakutambua kuwa yupo mtu /kitu/nguvu kinachokufanya upumue!
Hakika mwaka unapoanza ni vyema kurudi na kutafakari upya kusudi lako duniani
Usiishi kwasababu upo tu na unapumua, ishi kwasababu unakusudi lililokufanya uwepo hapa.(uishi)
Tumia siku ya mkesha wa mwaka mpya kwa mafanikio makubwa, malengo na mafikirio ya zaidi ya ulipo
Fanya ibada kamili kwa kudhamiria, nena yaliyo chanya ndani yako nawe utakuwa nyota ing'aayo usiku na mchana
Badili mwenendo wa maisha yako, badili namna yako, fanya maamuzi leo, nawe utakuwa kileleni siku zote na Mungu atakubariki kwa maana unatimiza kusudi lako la kuwepo duniani.
"HAPPY NEW YEAR 2018"