Mwaka Kesho Mtaipigia Staz Makofi

Kichankuli

JF-Expert Member
Dec 18, 2008
887
189
Baada ya Maxcimo kuchezeshwa Nzawisa na Chamukwale na kukubali kipigocha bao mbili bila na Bakongo, aliibuka jana na kudai kuwa wale mashabiki ambao walijitoa kimasomaso na kuibeza timu yake iliyoboranga katika mchezo huo wa kirafiki mwaka kesho watakuwa ni haohao ambao wataipigia makofi na kuchekelea ushindi itakaokuwa inawapa.

Napata shaka kuyameza maneno ya matumaini yaliyoongelewa na Macsimo kwa sababu ana miaka minne sasa tangu awasili na kukabidhiwa mikoba na haya ndiyo matokeo yake. Kibaya zaidi ni tabia yake ya kuwachukia wachezaji wake huku akitoa sababu za kugubika za wachezaji hao kukosa nidhamu.

Kwenye kukabiliana na athari za UKIMWI tunaaswa kuishi kwa matumaini, iwe hivyohivyo tena na kwenye soka mchezo tunaoupenda? Wadau mnasemaje
 
Back
Top Bottom