Mwaka huu TANESCO watashusha bei kwa 7% tunawasubiri

tikatika

JF-Expert Member
May 6, 2011
2,330
4,119
Mwaka jana tarehe 29.2 .2016 ahad ya TANESCO ni kutupunguzia umeme kwa 7% mwaka huu. Kauli hiyo ilitolewa na mhandisi Mramba wakati anatoa tangazo la kushushwa kwa bei ya umeme kwa 1.1%.

Baada ya kutumbuliwa nafikiri anayebadiri nafasi yake atatekeleza mpango huo wa TANESCO. Sitaki kuamini drama hii inayochezwa sasa hivi ya kutaka kutupandishia umeme kwa 18% nyuma ya ahadi ya kupunguziwa kwa 7% .

Huu binafsi naona ni mchezo wa kisiasa. Na kama tutaendelea kuendesha mashirika yetu kisiasa kama hivi kamwe tusitegemee kukua kwa mashirika yetu. Hebu jaribu kufikiri kidogo hii drama ilivyo.

Mwaka jana tarehe tajwa hapo juu walisema wanashusha umeme kwa bei ya 1.1 na kutoa ahadi ya kushushwa kwa 7% mwaka huu wakitoa sababu kuu kwamba TANESCO imetua baadhi ya mizigo kutokana na uwekezaji wa serikali katika mifumo ya gesi. Sasa tujiulize huo uwekezaji umesitishwa?

Kwanini watake kutupandishia kwa 18%? Watanzania kweli huu utashi tunaoutumia ndio tuliopewa na Mungu au kuna watu wanatuendesha? Takribani miezi kumi iliyopita walishusha bei iweje ipande sasa hvi?

Tena inapanda kwa kupaa? Kweli mashirika yetu yana mipango ya muda mrefu? Tutegemee mafanikio kwa mipango hiii? Kiukweli kuna sehemu tumekosea hatuwezi kuchezewa hivi na wanasiasa harafu tukapiga makofi. Kuna tatizo vichwani mwetu. Na huenda watawala wameona IQ zetu ndio maana wanatuendesha wapendavyo.

Yote kwa yote nategemea kushushwa kwa bei ya umeme kwa 7% kama ahadi ya TANESCO ilivyokua mwaka jana. Shirika ni lilelile serikali ni ileile hakuna kilichobadirika. Labada kama sisi hatuna kumbukumbu kudai ahadi zetu. Hii ya kupanda na kupigwa stop mimi naona ni mchezo wa kisiasa tuone wanatuhurumia ili tusidai ile 7% waliotuahidi mwaka jana kutushushia. Mimi nakumbuka nataka serikali itekeleze.

Angalia kauli ya mramba hapa!

 
Winders will never end,
Au Mramba alisoma vibaya ilitakiwa aseme wanampango wa kupandisha gharama za umeme kwa 7% badala ya kupunguza.
 
Hii nchi Wanasiasa wetu na Watendaji wakubwa wa Serikali na Watendaji wakuu wa Mashirika wanatugeuza watanzania kama mataahira wao!

Hivi kama kauli hiyo ya huyo Mramba aliyotoa hadharani, halafu hivi sasa akataka kufanya vice versa na kutaka kutupandishia bei ya umeme?

Kwa mazingira hayo tunalazimika kumsupport Magu kwa kuwatumbua watu wa dizaini hiyo......
 
Hukumu ya ya ICSID ya kuamuru Tanesco iwalipe SCB HK imesababisha story kushuka bei umeme iwe ya kupandisha bei umeme. Sasa mtakatifu aseme mgao wa pesa ya Escrow ilikua ni wizi lasivyo na yeye alifaidika uo mgao kwenye uchaguzi uliopita
 
Wameshindwa kesi na IPTL na wanadaiwa mabilioni ya fedha. Unadhani watalipaje? Ukweli tuzugezuge tu na kutumbuana kisiasa lakini mwisho wa siku bei ya umeme itapanda tu!
 
Back
Top Bottom