Mwajiriwa wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar azungumza kuhusu kupiga kura

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,792
31,804
Mohammed Ghassani

Aliyenitumia alitaka niihariri kwanza kisha kama naona inafaa niiweke hapa. Mimi sijaona haja ya kuihariri. Naiweka kavukavu kasoro jina lake tu:

"A.alaykum. Natamani ningeandika kama post yangu ila kwa usalama wangu napitia kwako ukiona inafaa kuiweka au pia kuihariri kabla.

Mimi ni mtumishi wa umma kupitia shirika la serikali.

Kushiriki katika kura ya Jumapili, 20 March 2016 nikuisaliti nafsi yangu. Siwezi kuisaliti nafsi yangu na nafsi za wanyonge walio wengi eti kwa kisingizo cha kulinda ajira yangu. Ajira. Sikuajiriwa kwa sifa ya kupiga kura. Kura imo ndani ya ridhaa ya nafsi yangu. Kura ni uhuru wangu.

Sitaki kwa sababu uchaguzi uliopita sikuona hekaheka za kulazimishwa. Iweje uchaguzi huu nilazimishwe. Uchaguzi uliopita sikuona bakora kuwatesa wanyonge. Uchaguzi huu, wanyonge wanateswa eti kwa kuwa wameyaamua yale wasiyoyaridhia wanga'ng'anizi wa madaraka.

Kama tume haiingiliwi katika maamuzi, basi na tume ya moyo wangu haiingiliwi katika maamuzi ya kwenda au kutokwenda kupiga kura. Kufukuzwa kazi kwa hili kutaacha historia katika uhai wa maisha yangu. Natamani niwe shujaa katika jambo hili. Siendi kupiga kura. Sipigi. Mnatosha na askari wanatosha kupiga kura. Wasipige watu tu, wapige kura. Jumapili ni siku yangu nzuri ya kupumzika.

Mungu ibariki Zanzibar.''
 
Waliopenda kupiga kura tumewaona wamepiga wewe ambaye hujapiga hukulazimishwa. Malalamiko yasiyokuwa na msingi haya.
 
Mohammed Ghassani

Yesterday at 9:51pm ·

Aliyenitumia alitaka niihariri kwanza kisha kama naona inafaa niiweke hapa. Mimi sijaona haja ya kuihariri. Naiweka kavukavu kasoro jina lake tu:

"A.alaykum. Natamani ningeandika kama post yangu ila kwa usalama wangu napitia kwako ukiona inafaa kuiweka au pia kuihariri kabla.

Mimi ni mtumishi wa umma kupitia shirika la serikali.

Kushiriki katika kura ya Jumapili, 20 March 2016 nikuisaliti nafsi yangu. Siwezi kuisaliti nafsi yangu na nafsi za wanyonge walio wengi eti kwa kisingizo cha kulinda ajira yangu. Ajira. Sikuajiriwa kwa sifa ya kupiga kura. Kura imo ndani ya ridhaa ya nafsi yangu. Kura ni uhuru wangu.

Sitaki kwa sababu uchaguzi uliopita sikuona hekaheka za kulazimishwa. Iweje uchaguzi huu nilazimishwe. Uchaguzi uliopita sikuona bakora kuwatesa wanyonge. Uchaguzi huu, wanyonge wanateswa eti kwa kuwa wameyaamua yale wasiyoyaridhia wanga'ng'anizi wa madaraka.

Kama tume haiingiliwi katika maamuzi, basi na tume ya moyo wangu haiingiliwi katika maamuzi ya kwenda au kutokwenda kupiga kura. Kufukuzwa kazi kwa hili kutaacha historia katika uhai wa maisha yangu. Natamani niwe shujaa katika jambo hili. Siendi kupiga kura. Sipigi. Mnatosha na askari wanatosha kupiga kura. Wasipige watu tu, wapige kura. Jumapili ni siku yangu nzuri ya kupumzika.

Mungu ibariki Zanzibar.''
Eeee mzee wangu Mohamed said naona umeamua kuzisambaza propaganda za Mohammed Khelef... Na huyu huyu jamaa ndiyo aliyeanzisha ule uwongo wa meli ya Mapinduzi 2 ni second hand. Na sijui zile picha ulizotuwekea wiki moja iliyopita na ukataka tuamini kama ni za Pemba wakati ni za Unguja na matukio yake yalikwisha kutukoa kama miaka 3 nyuma. Insuch away kwenye zile picha hata picha ya michenzani Unguja hukuijua ambayo ndiyo easy landmark.
pole sana kura zimeshapingwa na tunasubiri kuapishwa Raisi
 
Mbona hii hata si habari; kupiga kura ni hiari. Hata wale walioenda kupiga kura na kuchafua karatasi za kura walifanya hivyo kwa hiari yao. Inawezekana kukawa na kura nyingi zilizoharibika kwa sababu hiyo. Hakuna uchaguzi ambao watu wote waliojiandikisha wameenda kupiga kura...
 
Kizibao,
Tuanze na hili la meli.

Ikiwa una ushahidi kuwa meli ni mpya nipatie na nitauweka kwenye blog
yangu mohammedsaid.com

Picha za wiki iliyopita ningeomba uniwekee nizione ndipo nitazungumza.
Mbona umechagua picha za kuzizungumzia vipi kuhusu hizo nyingine?

Hili la kupigwa kura si muhimu muhimu ni uchaguzi wenyewe wote.
Tatizo lipo hapo.

Halikadhalika kuapishwa hili si jambo muhimu kwani hivyo alivyo bila
ya kuchaguliwa ni raisi tayari.

Angalia kura hizo hapo chini nadhani zina ujumbe muhimu:

2016%2B-%2B1

Screenshot_2016-03-21-06-05-41.png
 
Mbona hii hata si habari; kupiga kura ni hiari. Hata wale walioenda kupiga kura na kuchafua karatasi za kura walifanya hivyo kwa hiari yao. Inawezekana kukawa na kura nyingi zilizoharibika kwa sababu hiyo. Hakuna uchaguzi ambao watu wote waliojiandikisha wameenda kupiga kura...
Mzee Mwanakijiji,
Kweli hayo uliyosema lakini huu uchaguzi wa Zanzibar hauingii katika
mfano huo.

Uchaguzi huu umerudiwa baada ya CCM Zanzibar kushindwa.

Naweza nikakurudisha nyuma zaidi katika historia ya chaguzi za Zanzibar
kuanzia 1995 ikiwa utapenda uone tatizo lilipo.
 
MM Kama haupo Bongo basi naweza kukwambia pole,na hiyo ndiyo Afrika.Huko wametishiwa kufukuzwa kazi endapo hawataenda kupiga kura.Hivyo unaangalia ubavu wako ukiona mambo magumu basi waenda kupiga kura hata kuiharibu,japo mpaka sasa hawajasema kama kun kura zimeharibika
 
Mbona hii hata si habari; kupiga kura ni hiari. Hata wale walioenda kupiga kura na kuchafua karatasi za kura walifanya hivyo kwa hiari yao. Inawezekana kukawa na kura nyingi zilizoharibika kwa sababu hiyo. Hakuna uchaguzi ambao watu wote waliojiandikisha wameenda kupiga kura...
MM naona umeamua kutukanisha intellect yako kuita maigizo ya machi 20 uchaguzi.
 
Uchaguzi huu umerudiwa baada ya CCM Zanzibar kushindwa.

CCM ilishindwa wapi? Weka matokeo yote ya Zanzibar nzima ya Oktoba 2015 kama unayo. Unasilikiliza porojo za seif shariff hamad ZA KUJITANGAZA.

Ulishaona wapi mtu anakuwa yeye ndiye mgombea uraisi,mjumlisha kura za nchi nzima na mjitangaza mshindi mwenyewe!!!!!

Kama alikuwa kashinda alikuwa na kiherehere gani cha kujitangaza si angesubiri tume imtangaze.
 
Tulipofikia kama taifa kwa kudanganya, lolote lawezekana.
Wala siamini chochote, aliyeandika na aliyeandikiwa na asiyeandika ma asiyeandikiwa.
 
Anaethetist,
Ulichosema ni kweli kuwa katika ulimwengu huu unatakiwa
uwe makini usiamini kila ukisomacho.

Lakini...
Tuko makini sana na tunaaminiwa na wengi.

Ukipenda pitia maandishi yangu mengine utajifunza kitu kwani
kuna waandishi na waandishi:

Ingia hapa:
mohammedsaid.com
 
Mbona hii hata si habari; kupiga kura ni hiari. Hata wale walioenda kupiga kura na kuchafua karatasi za kura walifanya hivyo kwa hiari yao. Inawezekana kukawa na kura nyingi zilizoharibika kwa sababu hiyo. Hakuna uchaguzi ambao watu wote waliojiandikisha wameenda kupiga kura...
MM, kwa taarifa yako ni kwamba wafanyakazi wote wa Pemba, walitakiwa kuwasilisha wizarani vitambulisho vyao vya kupiga kura, yakachuuliwa majina na nambari ya vitambulisho, na wakaambiwa kuwa siku ya kupiga kura kutatolewa ithibati ya kuwa "wewe umepiga kura". Alipoulizwa afisa mmoja alisema ni kweli kuwawataka wafanyakazi wapeleke vichinjio vyao, lakini kwa lengo la "kuhakiki wafanyakaazi hewa." Na hata Unguja wafanyakazi wengine (walimu kwa mfano) walipewa amri ya mdomo, "kutoka juu", kuwa wanatakiwa wakapige kura.
Kwa ufupi MM, yanayotokea visiwani ni wa visiwani pekee wanayoyajua. Kwenye uchaguzi wa 1995 wafanyakazi walifuatiliwa kwenye vishina vya kura, na kila aliyejulikana kuipigia CUF alikiona cha moto. Mara nyingi hufikia hatua hadi ya kupuuza maandiko ya kaka yangu Mohammed Said, lakini kwa hili niko pamoja naye kwani na mimi ni muathirika wa tukio hili.
 
CCM ilishindwa wapi? Weka matokeo yote ya Zanzibar nzima ya Oktoba 2015 kama unayo. Unasilikiliza porojo za seif shariff hamad ZA KUJITANGAZA.

Ulishaona wapi mtu anakuwa yeye ndiye mgombea uraisi,mjumlisha kura za nchi nzima na mjitangaza mshindi mwenyewe!!!!!

Kama alikuwa kashinda alikuwa na kiherehere gani cha kujitangaza si angesubiri tume imtangaze.
naona bora ukatafute mtu akusukundu tu hivi wee unaona Tume ya uchakuzi watamtangaza mpizani wakati tume ya uchaguzi wenyewe ti tawi la ccm
 
Mzee Mwanakijiji,
Kweli hayo uliyosema lakini huu uchaguzi wa Zanzibar hauingii katika
mfano huo.

Uchaguzi huu umerudiwa baada ya CCM Zanzibar kushindwa.

Naweza nikakurudisha nyuma zaidi katika historia ya chaguzi za Zanzibar
kuanzia 1995 ikiwa utapenda uone tatizo lilipo.
Heshima yako MS . Tudiaha hio historia kwa manufaa ya wengi tuliopo humu. Dhulma iliuofanyika huko visiwani hata ccm nafsi zao zinajua
 
Mohammed Ghassani Aliyenitumia alitaka niihariri kwanza kisha kama naona inafaa niiweke hapa. Mimi sijaona haja ya kuihariri. Naiweka kavukavu kasoro jina lake tu:

"A.alaykum. Natamani ningeandika kama post yangu ila kwa usalama wangu napitia kwako ukiona inafaa kuiweka au pia kuihariri kabla.

Mimi ni mtumishi wa umma kupitia shirika la serikali.....

Mungu ibariki Zanzibar.''

Mbona umemtaja tena wakati ili kuwa siri kati yenu? Umeamua kuhatarisha maisha yake? Au utunga mwenyewe hii habari?
 
Tujitegemee,
Hiyo habari siri iko kwa mwandishi tu jina lake ndilo limehifadhiwa.

Barua yenyewe ni bayana iko FB na aliyeiweka hadharani ni Mohamed
Ghassani.

Mimi nimeinakili FB na kuiweka katika blog yangu mohammedsaid.com
 
Back
Top Bottom