BURUDIKA
Member
- Dec 30, 2013
- 91
- 8
Habari wana JAMII FORUM,
Naomba nianze kutanguliza samahani kwa wote nitakaokuwa nimewakwaza kwa namna moja au nyingine.
Mimi ni kijana nilie maliza degree ya Biashara (BBA) ktk chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) pia nina ujuzi wa Graphics Design ambao nilisomea UNIVERSITY OF DAR ES SALAAM COMPUTING CENTRE (UCC).
Nimekuja kwenu wanajamii wote muweze kunisaidia kwa na namna yeyote ile, yani ushauri na hata kama unaweza kuniajiri ktk kazi yoyote ile sio mbaya au kama una mtu ataweza kunisaidia basi usisite kunijulisha kwa e-mail address hii apa (munguku84@gmail.com).
Nimeamua kufanya hivi baada ya plani zangu kugonga mwamba kama nilivyoeleza apa chini.
MAELEZO YA PLANI ZANGU NIKIWA CHUONI
Nilipo anza chuo kikuu mwaka 2010 mwezi wa tisa nilikuwa na mawazo ya kujiwekea pesa ili nikimaliza chuo niweze kufanya biashara uku naendelea kutafuta kazi taratibu, mawazo hayo hayakuweza kutimia kwa mwaka huo wa kwanza kwasababu nilikuwa mgeni na BAJETI za maisha ya chuoni na pesa tuliyokuwa tukipewa(BOOM) ilikuwa ndogo hivyo sikuweza kutimiza malengo hayo kwa mwaka wa kwanza.
Nilipofika mawaka wa pili pesa ya matumizi(BOOM) iliongezwa na nikaona ndio muda muafaka wa kutimiza malengo yangu na nikaanza kujiwekea pesa lakini kwa kuwekeza kwenye kilimo cha mpunga huko kilombero mkoani Morogoro.
Boom la mwanzo wa mwaka wa masomo huwa na kiasi kingi na nilikuwa nikiweka laki mbili na nusu na BOOM zilizofuata nilikuwa nikiweka laki mbili tu.
Hizo pesa sikuwa naifadhi mwenyewe bali nilikuwa namtumia rafiki yangu ambaye nilijuana nae wakati nimemaliza kidato cha sita nilipokuwa nafundisha shule moja hivi ya sekondari ktk wilaya ya Kirombero. Rafiki yangu huyo pia nilimfanya kama mdogo wangu kwsababu alikuwa ni mdogo kwangu lakini alikuwa na akili za kusimamia mashamba hasa ya Mpunga kwasababu ndio ilikuwa shughuli zake uku anasoma.
Nilimtumia vizuri na nikalima ekali 3 za Mpunga na yeye alilima ekali 3 za Mpunga, tulitumia gharama nyingi sana, tukiwa na matumaini kuwa tukivuna tutaanza kufanya biashara ya kusafilrisha mchele kuja Dar es salaam na kuuza wilayani humo pia.
Nilijinyima sana nikiwa chuoni na nilikuwa naishi maisha magumu kwasababu nilijua nafanya jambo ambalo lingenisaidia ktk maisha yangu ya baadae hasa baada ya kumaliza masomo yangu ya chuo kikuu.
Nilipo maliza masomo nilirudi na kwenda kuangalia kilichopatikana shambani ndipo apo nilitamani kulia ndugu zangu. Tulivuna wote ule Mpunga na kufanya taratibu za kuuweka kwenye magunia na nikajikuta nimepata GUNIA 5 za mpunga kwenye hekali 3 na rafiki yangu nae akapata idadi ya gunia hizohizo 5, kkwahiyo hekali 6 tukapata MAGUNIA 10 ya mpunga na matarajio yetu ni kupata magunia Magunia 30 kwa hekali 3, jumla kwa hekali zote ni magunia 60.
Nilikubaliana na matokeo kwasababu nilishuhudia kilichopatikana kwa macho yangu na hizo gunia 5 za mpunga nilikoboa na kuuza na kupata laki 2 na nusu yani hata ROBO ya gharama nilizotumia hazikufika wana JF. Nilikuwa na STRESS muda wote nikifikiria sina pakuanzia na malengo yangu yameshapotea.
Kutokana na kushindikana kwa PLANI hiyo ndipo nilipo amua kuanza zoezi gumu linalohitaji uvumilizu na subira la kutafuta kazi za kuajiriwa hapa Dar es salaam.
Mpaka sasa juhudi hizi za kutafuta kazi naona zimenishinda kwasababu nimetuma maombi sana ktk makampuni mbalimbali na kuitwa kwenye usaili lakini sijawahi kupata kazi na sehemu nyingine niliombwa pesa lakini nikashindwa kutoa kwasababu sina pesa hizo.
Narudi kwenu wana JF nikivaa bango la MFICHA UCHI HAZAI hivyo basi naomba tena sana kama unaweza kunisaidia au unafahamu kunielekeza kwa mtu yeyote wa kunisaidia wasiliana nami kwa e-mail address munguku84@gmail.com.
Nakaribisha maoni na ushauri wako sasa.
Asanteni sana wana JF.