Mwaikimba arudisha Kilimanjaro Stars


K

Konaball

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Messages
2,365
Likes
918
Points
280
K

Konaball

JF-Expert Member
Joined Mar 11, 2009
2,365 918 280
KOCHA wa timu ya taifa Jan Poulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 22 uku akimrudisha kundini mshambuliaji Gaudence Mwaikimba na Juma Nyosso ambao walitemwa kwa kipindi kirefu katika kikosi cha Mbrazil Marcio Maximo.
Mwaikimba mshambuliaji wa zamani wa Yanga alikuwa mmoja wa washambuliaji tegemeo wa Stars chini ya Kocha, Marcio Maximo raia wa Brazil, hata hivyo baadaye alimuacha mshambuliaji huyo kutokana na kushuka kiwango na baadae kufungashiwa virago na Yanga.
Hata hivyo mchezaji huyo ambaye awali alikuwa kipenzi cha Maximo kutokana na umbile lake amekuwa lulu kwenye timu ya Kagera anayochezea hivi sasa na aliweza kumshawishi Poulsen amrudishe kundini baada ya kuonyesha kiwango kizuri kwenye mzunguko wa kwanza wa Ligi uliomalizika mwishoni mwa wiki.
Wachezaji wengine walioitwa kwenye kikosi cha Kilimanjaro Stars ambacho kitashiriki michuano ya Chalenji iliyopangwa kuanza Novemba 27 hapa nchini ni mlinda mlango Juma Kaseja (Simba), Shaban Kado (Mtibwa) na Said Mohamed wa Majimaji. Wengine ni Shedrack Nsajigwa, Erasto Nyoni, Stephano Mwasika, Shamte Ally, Idrisa Rajabu, Shaban Nditi, Henry Joseph (Kongsvinger- Norway), Nurdin Bakari, Jabir Aziz, Nizar Khalfan (Vancouver Whitecapes -Canada), Salum Machaku, Mohamed Banka na Kiggi Makasi.Wengine ni Dan Mrwanda (DT Long - Vertinam), Mrisho Ngasa, John Boko, na Thomsa Ulimwengu anayesaka soka la kulipwa nchini Sweden.
Akitangaza kikosi hicho Poulsen alisema baadhi ya wachezaji hao pia wataunda kikosi cha timu ya taifa Taifa Stars kitakachocheza mechi ya taifa ya kirafiki Novemba 17 kujiandaa na michuano ya kufuzu fainali za mataifa ya Afrika baadae mwakani itakayofanyika Gunea.
 

Forum statistics

Threads 1,235,132
Members 474,353
Posts 29,212,863