Mvutano wa gesi Mtwara dalili ya wananchi kukata tamaa

Mvutano wa gesi Mtwara dalili ya wananchi kukata tamaa

shadow recruit

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2011
Posts
1,844
Reaction score
384
Mvutano wa gesi mtwara ni dalili ya wananchi wa kusini kukosa imani na serikali yao katika kusimamia rasilimali za taifa,huu ni wakati wa serikali kujitathmini ni vipi watajidhatiti kusimamia rasilimali za taifa kama meno ya tembo na madini,ili kupunguza wimbi la wananchi kuzuia rasilimali za maeneo yao.
 
Waziri Simbachamwene anajaribu kuwauzia wana Mtwara mbuzi ndani ya gunia.

"Baada ya gesi kuanza kuzalishwa na kuuzwa, kazi ya wananchi wa Mtwara kupitia halmashauri zao za wilaya itakuwa ni kusoma mita kuangalia kiasi gani kimekwenda Dar es Salaam na kimeingiza fedha kiasi gani na kukokotoa asilimia zao ambazo lazima zirejeshwe kwa ajili ya maendeleo yao," alisema Simbachawene

Hivi tatizo la umeme Tanzania linatokana na kutokuwepo Bomba la gesi toka Mtwara???

Kweli Serikali ya CCM ina vituko vya mwendawazimu.

"Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amesisitiza kuwa mgogoro na vurugu zinazoendelea mkoani Mtwara kuhusu gesi unachangiwa na wanasiasa.Alisema kuwa watu hao aliodai wanakosa uzalendo na utaifa, wanalenga kuhakikisha tatizo la umeme linaendelea kuwepo nchini hadi uchaguzi mkuu ujao ili wapate ajenda ya kisiasa jukwaani."
 
Ni uvivu wa kufikiri wa baadhi ya viongozi..kazi ya vyama vya siasa ni ku create awareness katika jamii juu ya mambo yanayohusu mustakabali wao,sasa wanavyosema vyama vya siasa vinapotosha wananchi kwa lipi hasa..wananchi wamekata tamaa kutokana na ufujaji wa rasilimali.
 
Waziri Simbachamwene anajaribu kuwauzia wana Mtwara mbuzi ndani ya gunia.

"Baada ya gesi kuanza kuzalishwa na kuuzwa, kazi ya wananchi wa Mtwara kupitia halmashauri zao za wilaya itakuwa ni kusoma mita kuangalia kiasi gani kimekwenda Dar es Salaam na kimeingiza fedha kiasi gani na kukokotoa asilimia zao ambazo lazima zirejeshwe kwa ajili ya maendeleo yao," alisema Simbachawene

Hivi tatizo la umeme Tanzania linatokana na kutokuwepo Bomba la gesi toka Mtwara???

Kweli Serikali ya CCM ina vituko vya mwendawazimu.

"Katika hatua nyingine, Naibu Waziri wa Nishati na Madini, George Simbachawene amesisitiza kuwa mgogoro na vurugu zinazoendelea mkoani Mtwara kuhusu gesi unachangiwa na wanasiasa.Alisema kuwa watu hao aliodai wanakosa uzalendo na utaifa, wanalenga kuhakikisha tatizo la umeme linaendelea kuwepo nchini hadi uchaguzi mkuu ujao ili wapate ajenda ya kisiasa jukwaani."


Yaani ukitaka kujua jinsi viongozi waliopo kwenye serikali hii walivyofilisika kimawazo wasikilize kauli zao, eti waziri mzima unajenga hoja kuwa wanasiasa hawataki tatizo la umeme liishe ndi maana wanagomea gesi. kwanza wanaogomea gesi si wanasiasa ni wananchi na sababu za kugomea gesi isitoke zimeshaelezwa kila sehemu na serikali imeshindwa kutoa majibu.

Sababu kubwa ya wananchi kugomea gesi isitoke mtwara ni usimamizi mbovu wa rasilimali za nchi walioushuhudia katika maenea tofauti ya nchi hii ambapo umewanufaisha viongozi wachache waliopo serikalini na kuwaacha wananchi wa maeneo yanayozunguka rasilimali hizo wakibaki kwenye lindi la umasikini.

Jambo hilo linaonekana litawatokea na wao dhahili kwani hata kabla ya hiyo gesi kuchimbwa, tayari kuna viongozi wameshachukua rushwa (akiwemo Ret. Gen. Mboma aliyeficha uswisi)kutoka katika makampuni ya uchimbaji, hivyo wananchi hawatarajii kunufaika tena na hiyo gesi zaidi itabaki historia tuu.

Simbachawene hajui kuwa matatizo yaliopo tanesco hayahusiani na gesi bali mikataba iliyoingiwa na viongozi wa serikali akiwemo bosi wake JK aliyesaini mkataba wa kwanza wa kinyonyaji wa IPTL dhidi ya Tanesco wakati huo akiwa waziri wa nishati na madini.

Hii nchi asikudanganye mtu sijui tutapitia mikataba upya, au tanzania hakuna wataalamu wa mikataba. Hii nchi watu wameamua kuifilisi, maana kama kungekuwa na mtu anataka kuipitia mikataba ya madini, asingewaongezea mkataba mwingine barrick baada ya mkataba wa kwanza kuisha, Pili kama wanasaini mikataba yenye masilahi kwa wananchi kwa nini wanaogopa kuiweka wazi.

Inasemekana hakuna mkataba mbaya na wa kinyonyaji kama wa gas ya mtwara walioingia na wachina ndio maana wakapewa mkopo fastafasta ili mambo yaishe haraka. ila mbele tutajua tu hata wakiichoma moto kuna siku tutaijua tu
 
Hayo ndiyo madhara ya ubagusi,kila kitu Dar,arusha,kilimanjaro na Mwanza.Vyuo vyote huko na Morogor😵na miundombinu na hali hii ya mvua.Usiombe usafiri kipindi kwenda mtwara,unaweza kulia na hata viongozi wetu hawajali.Kuna sehemu inabolewa barabara za zamani na kujengwa mpya lakini tazama kusini,hali inasikitisha.Sera zenu za ubaguzi zitaigharamu nchi yetu
 
Kama kuupata ukweli wameshaupata na kama laana ya wanachi ipo basi awa viongozi wa serikali wataipata tu na mbona sisi wananchi tuko wengi kiasi kwamba kama tunasema wote kwa sauti moja kuwa hiki kitu hatutaki lazima wabadilike na ingelikua vizuri kama sehemu zote za tanzania kuwaonyesha kuwa tumechoshwa na hawa vuongozi ''eti kazi yao itakua kusoma mita tu ni ujinga mkubwa sana huu ina maana umeme ukizalishwa mtwara hauwezi kupelekwa sehemu zote za tanzania na kumaliza hilo tatizo la umeme simbachawene?

Au ili tatizo la umeme liishe ni lazima umeme uwe unazaliswa dar es salaam??? Mawaziri jaribuni kufikiria kauli zenu ambazo ni za kinafiki na mnachokitafuta katika hili mtakipata kwa sababu wanasiasa wenzenu mnawaona wanatafuta umaarufu nyie wanafiki mnatafuta nini?
 
kama kuupata ukweli wameshaupata na kama laana ya wanachi ipo basi awa viongozi wa serikali wataipata tu na mbona sisi wananchi tuko wengi kiasi kwamba kama tunasema wote kwa sauti moja kuwa hiki kitu hatutaki lazima wabadilike na ingelikua vizuri kama sehemu zote za tanzania kuwaonyesha kuwa tumechoshwa na hawa vuongozi''...

Hilo nalo neno.
 
Wananchi tumeshajifunza kutokana na Tanzanite na Dhahabu mnazoiba nyie mafisadi na makaburu na kutuachia mashimo Gesi haitoki Mtwara mpaka kieleweke tukimaliza issue ya gesi tunaamia kwenye Tanzanite ambayo mnakaribia kumaliza na Dhahabu sasa hivi lazima tunufaike na rasilimali zetu sio nyie wenyewe na watoto wenu hata mkitumia mabomu na vitu vyenye ncha kali hatuogopi
 
Back
Top Bottom