Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,411
Zaidi ya kaya 1394 za mitaa minane ya kata ya Nyegezi jijini Mwanza,hazina makazi kufutia mvua kubwa iliyoambatana na upepo mkali kuezua mapaa ya nyumba 61,huku waathirika wa mvua hiyo wakiiomba serikali kuwapa msaada wa haraka wa chakula na mahema kwa ajili ya kujisitiri na mvua zinazoendelea kunyesha.
Nyumba zilizoezuliwa mapaa yake kutokana na mvua hiyo ni za mitaa ya Ibanda relini,Pasua,Swila na Mnara wa Vodacom,ambapo baadhi ya waathirika wa mitaa hiyo wameiomba serikali kupitia kamati ya maafa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Nyamagana kuharakisha misaada ya kibinadamu.
Afisa Mtendaji wa kata ya Nyegezi Charles Muso akatoa ushauri kwa wananchi kuhakikisha wanajenga nyumba imara.
Mkuu wa wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza Mary Tesha Onesmo ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya maafa wilayani humo mbali na kutembelea kaya zilizoathirika kwa mvua hiyo kwa ajili ya kuwapa pole,amesema serikali imetoa shilingi milioni tatu kwa familia hizo kwa ajili ya kujikimu,huku kila familia iliyopatwa na maafa hayo ikipatiwa kilo 15 za unga.
Hakuna mtu aliyepoteza maisha kutokana na mvua hiyo.