Mvua yasababisha maafa Dar

Ashura9

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
740
485
MVUA zinazoendelea kunyesha nchini zimeendelea kuleta madhara baada ya watu wanne kupoteza maisha na wengine sita kujeruhiwa. Jijini Dar es Salaam mvua iliyonyesha kwa takribani saa tano mfululizo, ilisababisha athari kubwa hasa katika maeneo ya mabondeni pamoja na nyumba na barabara kujaa maji.
Hali ilikuwa mbaya jana majira ya asubuhi kutokana na mvua kubwa iliyoanza kunyesha tangu saa tisa usiku hadi saa tatu asubuhi. Mvua hiyo ilisababisha maeneo mengi, ikiwemo huduma muhimu kama barabara kujaa maji na kushindwa kupitika vizuri.

Katika eneo la Makumbusho Manispaa ya Kinondoni, njia ya kuingia kwenye kituo cha daladala ilijaa maji, kiasi cha magari kushindwa kupita, hali iliyosababisha msongamano mkubwa wa magari katika Barabara ya Morocco - Mwenge.

Aidha, katika maeneo ya mabondeni yaliyopo Barabara ya Kilwa kando ya mto Kizinga Manispaa ya Temeke, kutokana na mvua hizo moja ya madaraja ya barabara hiyo yalikatika na kusababisha maji na michanga kuingia kwenye nyumba zilizo kando na mto huo.

Wakati mwingine huwa sikielewi Kiumbe kinachoitwa "Binadamu" ni wabishi wanaposhauriwa haya ndio matokeo:

chanzo: Times fm

Tatizo watu wanang'ang'ania kuishi dar wakati mji wenyewe umekaa tuu bila npangilio…!! Hali hiyo unakaa mambonden umeambiwa si chini ya mara 5 utoke huko ukaamua kwenda mahakamani kupinga ukidhani unaikomoa serikali alafu linakuja janga kama hilo
 
Tatizo ya matatizo kutatuliwa ki siasa..
Afu watajitokezA kutoa msaada kwa wahanga wa mafuriko
 
Hivi huyo mbunge wa CUF aliekwenda mahakamani kuweka zuio la watu kuhama mabondeni na akashangiliwa sana na wakazi wa mabondeni, amepeleka msaada gani kwao? Maana jana tena watu hao hao wanaiomba serikali eti iwape msaada!
 
12573820_1010022375743689_807078294649668398_n.jpg

Picha sio ya tukio la mvua za wiki hii.......
 
Tatizo watu wanang'ang'ania kuishi dar wakati mji wenyewe umekaa tuu bila npangilio…!! Hali hiyo unakaa mambonden umeambiwa si chini ya mara 5 utoke huko ukaamua kwenda mahakamani kupinga ukidhani unaikomoa serikali alafu linakuja janga kama hilo
Mkuu unafiki Wa chagadema ndio umesababisha yote haya.

Vinajifanya vinajua kutetea wananchi kumbe unafiki tupu
 
Dawa chochote kitakachowakuta serikali ikae kimya maana vichwa vyao ni vigumu vichwa vyao hawana totauti na nyumbu Wa ukawa
 
Back
Top Bottom