kipapi
JF-Expert Member
- Sep 13, 2016
- 1,056
- 1,374
Wakuu habari za swaum,
Kwa wale waliofunga kama mimi na eid Mubarak kwa wanaokula sikukuu siku ya leo. Ama kwa hakika mimi kwa mtazamo wangu kwenye suala la muandamo wa mwezi naona leo (Jumapili) ilipaswa iwe sikukuu kwa dalili na sababu zangu zifuatazo;
1.Mvua inayoendelea kunyesha leo ni dalili kabisa ya kuwa mwezi umeandama jana, wajuzi wa mambo ya mwezi wamenithibitishia kuwa mwezi uliandama ila haukuonekana, leo asubuhi nilionana na mzee mmoja mashuhuri kwa shughuli za uvuvi pale ferry sokoni akanambia kwa ufupi tu "kwa dalili za Jana mwezi uliandama ila haukuweza kuonekana" na kwakuwa Tanzania kuna baraza kuu yaani (BAKWATA) kiitifaki tunabidi tusubiri tamko lao kama ilivyo ada maana ukiipinga BAKWATA sawasawa na kuipinga serikali.
2.Ikiwa kitovu na chimbuko la uislam, alipozaliwa mtume Muhammad (S.A.W), ilipoteremshwa Qur'an tukufu katika nchi ambayo ndio tunaenda kufanya hijja na nchi ambayo baadhi ya miji yake imetajwa mpaka kwenye Quran leo hii wanakula Eid el Fitr.
Hitimisho:
Tuendelee kuzingatia itifaki maana leo uonekane usionekane lazima kesho tule Eid maana tunasubiri kuonekana sio kuandama.