Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,874
- 7,650
Kuna kila dalili mvua hii ilioanza kunyesha majira ya saa moja kasoro asubuhi hii hapa Mtwara ikaleta madhara.
Na hii ni taarifa iwafikie wenye mamlaka hapa Mtwara mjini pamoja na wilaya za Mkoa wa Mtwara kuwa tayari kwa msaada wowote wa dharura ikibidi.
Maeneo ya Kiangu tayari yameshaanza kufurika maji huku Maeneo ya Mangoela na yenyewe yakiwa katika hatari ya mafuriko. Maeneo ya Jirani na Villa Park, Mduleni yamefurika pia.
Maeneo ilipo shule ya MEDI, Shangani yamefurika.
Mamlaka zitilie mkazo kuondoshwa kwa takataka zilizofurika kwenye madampo ambayo yapo jirani kabisa na makazi ya binadamu ili kuepuka milipuko ya maradhi ya kipindupindu.
Mvua hii inakwenda sambamba na Radi Kali za mwanga pamoja na Radi za Miungurumo na haijakatika tangu saa moja kasoro hadi muda huu naanzisha thread.