Muziki wa Singeli uko wapi siku hizi?? Pumzi imekataa au ndo ulikuwa upepo ka tulivyosema??

barafuyamoto

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
32,375
29,732
Habari!
Kama kichwa cha habari kinavyouliza, mziki huu wa singeli ulikuja kwa kasi ya ajabu na kuna watu walidiriki kusema sasa huu ndo mziki utakaodumu muda mrefu, kwamba ndio aina ya muziki mpya nchini kwa vijana kujiachia, ila kiukweli toka singo kali za singeli zitoke, hamna kipya kabisa na pia wale wasanii ambao walidhaniwa ndio nembo ya singeli wamepotea kabisa, yaani wanapumulia ktk machine!

Utabiri wetu tuliosema singeli ni UPEPO tu unaopita naona unatimia.
Namalizia kwa kipande hiki cha darasa, UNATAKA KUKIMBIA NA HUNA BREAK, WHAT DO YOU EXPECT......
Naona singeli baada ya VIROBA kupigwa BAN nayo imepotea, turudini sasa kwenye miziki ya maana, ikiwezekana miziki ya 2005 under ipigwe mwanzo mwisho.
 
mikono juu mwendo wa mateka mikono juu

Ee bwana ee. Maafande wakikamata wahuni wanawaimbia huu wimbo mi huwa nacheka tu aisee.

Mziki bwana una nguvu ya ajabu sana. Huwa najiuliza kwa nini mtoto mchanga akiskia mziki huanza ku-swing.

Nashindwa kuelewa kwa kweli.
 
Ee bwana ee. Maafande wakikamata wahuni wanawaimbia huu wimbo mi huwa nacheka tu aisee.

Mziki bwana una nguvu ya ajabu sana. Huwa najiuliza kwa nini mtoto mchanga akiskia mziki huanza ku-swing.

Nashindwa kuelewa kwa kweli.
Muziki ni hisia mkuu
 
Nyinyi ndo mliopenda singeli kwa ajili ya nyimbo ya Man Fongo Hainaga ushemeji, sasa kachuja mnasema singel imekufa ila kwa sisi tunaojua singel ilipoanzia bado tunaendelea kupata ladha murua
 
Back
Top Bottom