Muungwana, ujana ni maji ya moto.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muungwana, ujana ni maji ya moto..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by FDR.Jr, Nov 18, 2009.

 1. FDR.Jr

  FDR.Jr JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2009
  Joined: Jun 17, 2008
  Messages: 1,335
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  JK ,umri usiwe kigezo tafuta wachapakazi [​IMG] WAKATI tuhuma za utendaji mbovu wa mawaziri ambao unadaiwa kuwa chanzo cha kukwamisha mkakati wa kasi mpya zikipamba moto, Rais Jakaya Kikwete amewapa matumini vijana kuwa akichaguliwa tena mwaka 2010, wazee hawatakuwa na nafasi katika serikali yake.
  Katika hotuba yake aliyoitoa kwenye mkutano wa vijana kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika jijini Dar es Salaam, uliohusu mpango wa uongozi wa Afrika (Africa Initiative), Rais Kikwete alisema: “Kama nitajaliwa kuchaguliwa tena (2010), nitahakikisha naubadilisha uongozi wa Tanzania kwa kuufanya kuwa wa vijana”.

  Hii inamaanisha kwamba, akifanikiwa kuchaguliwa tena kipindi kijacho atatoa nafasi kubwa kwa vijana na kuifanya serikali yake kuwa ya vijana tofauti na sasa ambapo asilimia kubwa ya mawaziri na maafisa wa ngazi mbalimbali ni wazee.

  Kauli ya JK ni changamoto muhimu kwa maendeleo ya taifa na hasa katika masuala ya ajira nchini, ingawa hatuna uhakika kama kweli vijana wataweza kufanikisha utendaji kwa kiwango kinachotakiwa na kwa mazingira salama kutokana na hulka ya vijana katika kushughulikia mambo.

  Ni dhahiri kwamba, hata kama ataweka vijana kwa vyovyote vile kutakuwa na wazee wa kupooza mambo kama alivyosema wakati anaingia madarakani akikumbuka maneno ya baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere kuwa, ukiwaachia vijana nchi itawaka moto.

  Kama kweli rais anajiandaa kuondoa wazee kwa sababu anataka vijana, awe makini kwani kuna wazee wenye uwezo wa kiutendaji na wapo vijana wasioweza kitu.

  Kuna ushahidi wa kutosha kwamba, hata walioko katika baraza lake la mawaziri safari hii kutokana na kazi walizopewa kuna ufa mkubwa kuliko hata za baadhi ya wazee wanaotumia uwezo na elimu yao vizuri kulisaidia taifa.

  Maana yake ni kwamba, suala si bora vijana ili kupata watu wenye elimu nzuri, uwezo kwa kutumia ujuzi wao na si bora vyeti, wenye uchungu na nchi yao na waliotayari kulitumikia taifa kwa moyo wote na kulinda rasilimali za umma.

  Pia kama kweli anataka vijana, asiangalie urafiki kupitia mtandao wa ushindi na mchakato huo uanzie kwenye uchaguzi wa wabunge kwa kuweka taratibu zinazowaondoa wazee waliokalia viti vya ubunge kwa muda mrefu na hawana mpango wa kuondoka kwa kisingizio cha kuwa wanapendwa na wananchi hata kama hawana mchango wowote na wengi wanagombea kwa ajili ya ndoto ya kupata uwaziri au unaibu waziri.
   
 2. M

  Mtu B JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 921
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni mkakati mpya wa kuombea kura 2010?
  Tulisikia "maisha bora kwa kila mtanzania". Kwa hiyo sasa kauli mbiu mpya ni "maisha bora kwa vijana" au vp?
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Nov 18, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  suala la umri limekuwa tatizo sana katika maendeleo ya nchi yetu, mimi nadhani JK alitakiwa a-focus kwenye quality ya watendaji kuliko kuzungumzia umri

  • tumekuwa sasa tunaona hata nafasi za kazi wanaweka age limit [moja ilitoka inasema 40-50 yrs] - wanasahau kwamba kuna over fifty walio wazuri sana na under fourty walio wazuri sana
  • Suala la umri limesababisha kukosa umakini katika maamuzi kwani baadhi yetu vijana tunasema wazee wamechoka na baadhi ya wazee wanasema vijana hawajakomaa - all these are nonsense!!! because we focus on minor staffs

  Wazo langu ni kwamba JK alitakiwa aweke mkazo kwenye ubora wa watu kuliko umri
   
 4. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #4
  Nov 18, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mimi nafikiri ujana isiwe kigezo cha kuchaguliwa kuwa kiongozi. BALI uwezo, umakini, uadilifu na uzalendo uwe kigezo mama katika kucagua viongozi wa nchi.
   
 5. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #5
  Nov 18, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mimi Nafikiri kigezo cha kuchaguliwa kiwe ujana kwa sababu zifuatazo.
  1.Wazee wameshindwa miaka karibu hamsini sasa

  2.Timu yetu haiendi kwa sababu ina wachezaji wa rika moja, hawa wazee miaka 5 hadi kumi wote watakuwa mameishiwa nguvu, hivyo kutoingiza vijana serikalini kwa sasa ni technical mistake kubwa sana.

  3.Vijana Ndio generation mpya ambayo kwa sasa inaendana na kasi mpya ya dunia ni ambao wanauwezo wa kujifunza dynamically tofauti na wazee ambao tayari haiwezekani kujifunza dynamically nawanatumia mafunzo yale waliyojifunza statically na ndio maana utashindwa kuwaelewa maamuzi yao kwa sababu wanarefence ya dunia wenda haipo kabisa ama imepitwa na wakati.

  Kuhalalisha pointi yangu hapo juu leo chukuwa hao wazee ,wachanganye na vijana wafundishe mambo ya ICT uone mzee alivyo statically configured.

  4. Dunia ya leo inahitaji wajuvi wa ICT ili kwendana na kasi ya dunia ,hawa wazee kasi hiyo hawawezi asilimia 90% kama wanajuwa kutumia simu tu ni kupiga na kupokea.Ndio maana utaona physically wanazunguka mikoani kuhutubia vitu na vitu ambavyo vingi vingefanyika remotely kwa kufanya Conference kwa IT.Wazee wanatumia resources ,nguvu nyingi, mda mwingi na output yake ni kiduchu.

  Wazee waachie ngazi mda wao umekwishapita kasi ya dunia hawaiwezi tena .
  Totally they have gone the way of Dinosaur
   
 6. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #6
  Nov 18, 2009
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,575
  Likes Received: 541
  Trophy Points: 280
  vijana wako active zaidi na wanawaza mambo makubwa mambo ya utandawazi kijana kama ameonyesha ukomavu wake kimawazo kiutendaji na ni hardworker nn kinazuia asipewe uongozi ,ila hawa wazee mmh mtu unawaza nimebakiza miaka 4 nife kwa amani
  how come
   
Loading...