Baraghash
JF-Expert Member
- Dec 18, 2012
- 2,713
- 1,789
Muungano uliokuwa na siha, heshima, uvumilivu na usawa baina pande mbili zilizoungana na waasisi wake(Nyerere/Karume) na kuoneshwa njia muruwa ilionyooka umeshuhudiwa kwenye kipindi hicho 1964- 1972 wakati huo mmoja waasisi wa muungano (Karume)alipokuwa bado yuko hai.
1.Karume hakuridhia Mkataba wa Muungano "Articles of Union" na kulikuwa hakuna shinikizo kutoka upande wa pili wa Muungano ambao wao waliuridhia - Kuheshimiana
1.Karume hakuridhia Mkataba wa Muungano "Articles of Union" na kulikuwa hakuna shinikizo kutoka upande wa pili wa Muungano ambao wao waliuridhia - Kuheshimiana
- Jumbe alipojaribu kuhoji tu muundo wa muungano ,maafa na madhila yaliomfika hayahitaji maelezo na hayatosahaulika.
- Kuna wakati Karume alimkatalia Nyerere kupeleka JWTZ kutoka Zanzibar kwenda kujiunga na wenzao kwenda Msumbiji( kwa mreno) na Mtukula kukabiliana Iddi Amin. Karume alimwambia Nyerere hakuna msaada wa roho.
- Mkuu wa Majeshi ya JWTZ na Kamishna wa Polisi (IGP)Zanzibar waliteuliwa na Karume. Zanzibar majeshi yaliongozwa na Brigadier Yussuf Himid na bara Brigadier Sarakikya. Polisi Zanzibar yaliongozwa na Kamishna Eddington Kisasi na bara Kamishna Elangwa Shaidi na akisaidiwa na Kamishna Hamza Azizi.
- Karume alipkuwa ana kaimu Urais Bara aliitisha mkutano wa hadhara Jangwani,Dsm,na jambo lisilo sahaulika pale alipowatangazia watanzania kuwa kuanzia siku ile huduma ya maji safi Bara ni bure na akapiga marufuku ulipaji wa maji. Aliwauliza wananchi nini maana ya kujitawala kama unalipia hata maji ambayo ni hidaya kutoka kwa mungu?
- Ubalozi wa Ujerumani ya Magharibi ambao kabla ya Muungano ulikuwa una uhusiano na Tanganyika ililazimishwa kufunga virago baada ya kuhoji kuwepo ubalozi mwengine wa Ujerumani. Nyerere alimuheshimu Karume na kukubaliana nae kuwa Tanzania haichauliwi marafiki
- Uhusiano na jumuia ya Afrika ya Mashariki , Zanzibar ilikuwamwanachama wa kujitegemea.
- Mswali ya fedha kila nchi ilikuwa na ya kwake. Waziri wa Fedha wa Bara Bw. Jamal alipojaribu kutoa rai ya kuwa na Account moja ya fedha za kigeni, Karume alimfukuza kama mbwa Ikulu Zanzibar