Muungano huu hatuutaki

wanachofanya hawa jamaa kwa waarabu ni sawasawa na wale watoto wanaokuwa sexually abused mpaka kufikia hatua ya kudhani ni wajibu wao kuwa abused...tuwaache watwana waende kwa mabwana zao kwa amani...
 

Poleni sana. Lakini mfahamu ukweli rahisi kuwa kama muungano utavunjika mtakuwa na wakati mgumu sana. Kuna faida nyingi ambazo hazionekani lakini tukitengana tu ndipo mtakapozifahamu. Halafu kuudai muungano kwani ni mpaka mchome moto makanisa? kwani maaskofu ndio walioleta muungano. Daini nchi yenu lakini kistaarabu.
 
Kama kuvunja muungano kutatatua matatizo kama rushwa, kupanda hovyo kwa bei za bidhaa(leo nimenunua mafuta ya taa kwa tshs 5000 kwa lita!), uongozi mbovu, upatikanaji wa nishati,udhaifu wa miundombinu n.k. nitakua tayari kuunga mkono jitihada hizo, tofauti na hapo itabidi nijifikirie kwanza. Hoja yangu ni kwamba Watanzania wenzangu tujifunze kuyaangalia matatizo tuliyonayo na namna ya kuyatatua badala ya kutafuta mengine ambayo ndio kwanza yanaonesha dalili zote za kutuongezea matatizo mengine.
 

Mkuu! hayo usiyahusishe kabisa na utaifa wangu kama mTg! Hata MMungu kaanza kuumba Utaifa ndipo ikafua kaweka utaratibu wa kuishi humo!
 
Waliochoma Makanisa watajulikanwa na mm nina imani kua waliochoma makanisa sio wale jumuiya ya MUAMSHO na kma ni wao waliochoma basi nitawaita wapumbavu mna hata mm sikubalini na kilichofanywa kwa hao rafiki zetu wa dini nyengine...ila ukweli ukidhihiri ubaya hujitenga na ukweli maisha yote huuma...na kuhusu suala kama sisi wazanzibari tukiondoka tutakufa na njaa ningependa kua sisi sio wa kwanza kufa kwa njaa kwani somalia na nyengine za afrika vp huko mbona hamushangai, na suala la nchi hii zanzibar ni nchi na itaendelea kua nchi mna mpaka umoja wa mataifa wanalijua hilo na tukiamua kudai kila kilicho chetu mbona hamuna pa kukimbilia mna kihistoria sisi tumeanza kutambulikanwa mwanzo kuliko nyinyi tanganyika...............................ZANZIBAR MBELE DAIMA...........................MUUNGANO TUUTAKAO UWE NA FAIDA KWA PANDE ZOTE MBILI..............MUNGU IBARIKI JAMHURI YA WATU WA ZANZIBAR, MUNGU IBARIKI JAMHURI YA WATU WA TANGANYIKA,MUNGU IBARIKI TANZANIA TUITAKAYO NA MUUNGANO TUUTAKAO.....AMIIIIIIIIIIIIIINNNNNNNNNNNNNN....
 
Ngojea nikufahamishe kitu kidogo mdogo wangu.....kwamba sisi Waislamu tumefundishwa kua kila jambo jema lazima umtangulize Mungu mbele na nina imani kua utaelewa mantiki yangu ya kusema ivo la kama hujaelewa nenda kwenye biblia yako itakuambiaje...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…