Muswada wa Katiba kupitishwa: CHADEMA wame-score asilimia 92 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muswada wa Katiba kupitishwa: CHADEMA wame-score asilimia 92

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by SubiriJibu, Feb 10, 2012.

 1. S

  SubiriJibu JF-Expert Member

  #1
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 26, 2009
  Messages: 1,131
  Likes Received: 779
  Trophy Points: 280
  Muswada umepitishwa.

  Vifungu vilivyoletwa kwa ajili ya marekebisho ni kwenye ibara ya 6, 12, 13, 17, 18 na 21.

  Jumla ni vifungu sita.

  TUmejikita kwamba mjadala mkubwa ulhus kifungu cha Mkuu wa Wilaya ambacho CHADEMA walitaka asiwemo badala yake awemo Mkurrgenzi wa Wilaya. Ni kweli kimeleta ubishi zaidi ya siku nzima kwani CCM hawakutaka kabisa Mkurugezi Wilaya, walitaka abaki Mkuu wa Wilaya.

  Kuna wanaoona kuwa CCM wameshinda kifungu hiki. Lakini ukweli ni kwamba hawakushinda kwani haikuwa hoja yao iliyoletwa bali ilikuwa hoja ya kupinga kuondolewa kuu wa Wilaya na kuwekwa DC.

  Hatimaye imekuwa kwamba kama ni hivyo basi wote DC na DED wawemo. Ukweli hapa ni kwamba CHADEMA hawajashindwa kwani waliyemtaka kawemo tena baada ya mgogoro mkubwa.

  Hivyo, kwa kifungu hiki tunaweza kusema mechi ni draw. Kwa vifungu vingine vitano bado CHADEMA walifaulu.

  Hii ina maana gani?

  Maana yake ni kwamba CHADEMA wamepata 5+0.5=5.5

  Hivyo kwa vifungu vile sita inakuwa 5.5/6=92%

  Ni wanafunzi wangapi wanaoata hizo maks katika mtihani wowote duniani ambazo kwa kiwango cha grade kokote duniani hiyo ni "Distinction" au "A".

  Kwa maana hiyo mjadala wa kile kimoja ilikuwa CHADEMA wanataka kupata 100%.

  Mimi nadhani ni ushindi mnono kuliko malelezo.
   
 2. MTAZAMO

  MTAZAMO JF-Expert Member

  #2
  Feb 10, 2012
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 12,534
  Likes Received: 5,685
  Trophy Points: 280
  Chadema is very organised!!
   
 3. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #3
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  binafsi nimependezwa sana hoja za CDM kupigania kuwepo kwa DED ukilinganisha na zile za CCM za kuwepo kwa DC
   
 4. nitonye

  nitonye JF-Expert Member

  #4
  Feb 10, 2012
  Joined: Dec 18, 2011
  Messages: 7,167
  Likes Received: 508
  Trophy Points: 280
  Ni ushindi kwa CDM kwa sababu hata hicho kifungu walichokuwa wanakililia wana CCM kwamba wawekwe ma DC kimekubaliwa kwa sharti kuwa kamati ndio ina nguvu ya kukataa au kukubali kuwatumia hawa ma DC
   
 5. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #5
  Feb 10, 2012
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mi nadhani ushindi wa CDM ni zaidi ya hizo asilimia 92 kwasababu hoja zao kuhusu MA-DC na MA-DED zilikuwa grounded wakati CCM kama kawaida yao hoja zao zilikuwa za ushabiki wa Kichama. Pia CDM wameendelea kujipambanua kwa wananchi kwamba wapo kwa maslahi ya nchi na sio chama! Viva CDM!!
   
 6. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #6
  Feb 10, 2012
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  weka basi vifungu vyote na uonyeshe kama source yake ni CDM.
  ila sidhani kama ni sahihi kushabikia vyama kwenye hili la katiba ni vizuri yaangaliwe maslahi ya Taifa kama Mh Mbowe alivyoweka sawa
   
 7. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #7
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  Hayati Mwalimu Nyerere aliwahi kuulizwa ni chama kipi cha upinzani kitaisumbua CCM baadaye, akajibu CDM. jibu hili liliwaduwaza sana CCM kwani walidhani angesema CUF , au NCCR. Wote mashaidi utabiri wake umetimia.
   
 8. D

  Dopas JF-Expert Member

  #8
  Feb 10, 2012
  Joined: Aug 14, 2010
  Messages: 1,151
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Hoja yako bomba, kuhusu maksi kwa sisteem ya tz sawa pia,
  ila kuna sehemu nyingine
  A+= 100,
  A= 98-99,
  A-= 95-97

  Hata hivyo bravoooooo Chadema, chama cha ukombozi wa watanzania
   
 9. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #9
  Feb 10, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Hatimaye leo Mswada wa Marekebisho
  ya Sheria ya Mabadiliko ya Katiba
  umepitishwa huku CHADEMA wakiwa
  hawana cha maana walichokiambulia.
  Bado Marais ndiyo wanaoteua Tume.
  Bado Mawaziri wa Katiba na Sheria ndiyo wanaoteua Sekretarieti ya Tume.
  Bado Wajumbe wa Bunge Maalum la
  Katiba wamebaki kama walivyokuwa
  katika Mswada wa awali. Bado Rais wa
  Zanzibar ana nguvu zile zile katika
  kusimamia maslahi ya Zanzibar kwenye mchakato huu. Bado Zanzibar ina
  nafasi zake zote zilizoingizwa awali
  katika kusimamia maslahi yake. Bado
  kura ya maoni itasimamiwa na
  kuendeshwa na Tume za Uchaguzi
  zilizopo. Bado ni kosa la jinai kuingilia au kuizuia Tume ya Katiba kufanya kazi
  zake. Sasa kununa na kususa kwa
  CHADEMA kumeleta mabadiliko yepi ya
  maana? CUF imedhihirisha tena
  ukomavu wake wa tokea awali. Waje
  tuwafunze siasa!
   
 10. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #10
  Feb 10, 2012
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Trick! huku ndiko kuachwa kwenye mataa. Maana immediate boss wa DED ni DC!
   
 11. The Spit

  The Spit JF-Expert Member

  #11
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 45
  Hata kama Jussa ni Mungu wako lakini bado unalazimika kum-quote kwa kuweka bandiko lake!!!...Ndo nini sasa huo upupu rudisha facebook ulipoichukua unatuchafulia jamvi!
   
 12. kingxvi

  kingxvi JF-Expert Member

  #12
  Feb 11, 2012
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 883
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hakuna lolote hapa kwani yalikuwa mashindano
   
 13. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #13
  Feb 11, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  “When the hunted knows
  how to hunt, the hunting game is no
  more!”
   
Loading...