Ni nani aliefanya utafiti Dodoma akagundua saa 12 asbh hakuna abiria hadi saa nane mchana. Yani ukikosa treni ya saa 11 asubuhi inabid ukae hadi saa nane mchana. Ukienda kwenye mabasi unakuta yamejaza...kuna kitu hapa.
Treni za mizigo zilikuja kuna ugumu gani uliopo kuanza kazi? Au watu wa Malori wanawasilisha michango yao katika ofisi za kuhujumu?
Kwa nini hakuna promo za SGR yetu kwenye vyombo vya habari kuongeza hamasa ya utumiaji.
Wekeni vivutio vya kitalii kwenye SGR, vituo vyake na njia nzima tutakuza uchumi kuliko hivyo mnavyobandika na kuonesha kila mara.
Asanteni
Yaan ratiba zao hazijakaa kufanya biashara hata ule uendeashaji wao bado sana .
Hivi inakuwaje mfano treni kama pale dodoma kushindwa kupaki kwa wakati mmoja maana pale Kuna handaki kwa ajili ya njia ya kushukia ni kitendo cha kuongeza kipande cha reli ili kuingia ndani ya stesheni kuliko pale treni inapochelewa kutulazimisha kusubiria kwa zaid ya mpaka lisaa .
Au pale moro Kuna njia ya kupitia juu kwanini zile njia za juu zisiwekewe mazingira treni mbili zikawa zinashusha kwa wakati mmoja? Hivi tukija fika mwanza itakuwaje maaana abiria inaonekana watakuwa wengi sana kuliko kiwango
Kwan trc imeshindwa Nini kuingia mkataba na jiji Ile stendi ya shamba iliyoko mitaa ya pale stesheni isihamie hata pale kwenye magodown ya mkandarasi au kushoto mwa stesheni ili kurahisisha usafiri kuliko sasa hivi tunavolazimika kubeba na boda.
Route
Trc ipunguzwe bei ya emu na zifanye KAZI kama express train tu kutoka tsh 150,000 mpaka 90,000 na 70,000
Huku business class ya ordinary ikiwa 60,000 kusiwepo na premium kwa ordinary .
Ratiba nzuri
Dar Dom dar = 11 asubuhi(emu express)
Dar-dom-dar = saa Moja asubuhi
Dar-dom- dar= saa nne asubuhi
Dar -dom- dar = saa Saba mchana( emu express)
Dar-dom-dar= saa Tisa mchana
Dar Dom dar = saa 11 mchana( emu)
Dar-dom- dar= saa Tano usiku