Msema yote
JF-Expert Member
- Mar 19, 2013
- 448
- 301
Ndugu zangu, Huku Musoma watu wanaendelea kuisoma namba na sasa wanautambua vyema ule wimbo wa ccm hasa kile kibwagizo kisemacho "CCM NI ILE ILE". Wazazi wenye wanafunzi wasomao shule ya sekondari Nyabisarye ambayo ni shule ya kata iliyopo katika kata ya bweri wameonesha masikitiko yao baada ya agizo kutoka katika uongozi wa shule hiyo kuwataka wawalipie wanafunzi wao pesa ya chakula shilingi elfu kumi kila mwezi kwa maana ya 10,000 *12 = 120,000 kwa mwaka kwa kila mwanafunzi kuanzia form one mpaka form 4.
Baadhi ya wazazi na wananchi wengine kwa ujumla wamesikitishwa na swala hili hasa wakikumbuka walivoahidiwa elimu bure form one mpaka form pasipo michango yoyote na wakadanganyika na kuamua kumpiga chini Mussa wao aliekuwa amedhamilia kuwavusha kuwapeleka katika nchi ya ahadi, ambapo katika uongozi wake mambo kama haya hayakuwepo na yalikuwa yakisikika wilaya au mikoa mingine lakini sasa imefikia kwao, hii inaitwa Kuacha mbachao kwa msaala upitao.
#HAPA KAZI TU