Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,042
- 10,787
MAHAMA ya Wilaya ya Musoma, mkoani Mara, imemuhukumu, Monica Onyango, kwenda jela miaka mitatu au kulipa faini ya Sh. 500,000, baada ya kumtia hatiani katika kesi ya kughushi i cheti cha kidato cha nne na kukitumia kupata ajira.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Karimu Mushi, baada ya kusikiliza ushahidi wa mashahidi watano wa upande wa mashitaka na mshtakiwa mwenyewe aliyekuwa akitetewa na wakili wa kujitegemea, Thomas Makongo.
"Mahakama imekuona una hatia kama ulivyoshitakiwa baada ya kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi watano wa upande wa mashitaka ambao haukuacha shaka yeyote’’ alisema Hakimu Mushi.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Erick Kiwia, aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa mshitakiwa ili iwe fundisho kwake na wengine wenye tabia kama hiyo.
Kwa upande wake, mshitakiwa aliiomba mahakama imuonee huruma kwa kuwa ana watoto wadogo anaosomesha na anategemewa na familia kwani mume wake ni mgonjwa huku akiwa ameshapewa adhabu ya kufukuzwa kazi.
Mshitakiwa alifikishwa mahakamani hapo na Jamhuri kwa mara ya kwanza Oktoba 6, 2015 na kufunguliwa mashitaka mawili ya kugushi cheti cha elimu ya kidato cha nne na kuwasilisha cheti hicho katika ofisi ya katibu tawala kisha kupata ajira katika Hospitali ya Mkoa wa Mara.
Hakimu Mushi alisema amezingatia utetezi wa mshitakiwa, hivyo anamuhukumu kulipa faini ya Sh. 300,000 au kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka mitatu kwa kosa la kwanza na kosa la pili kulipa faini ya Sh .200,000 au kwenda jela miaka mitatu.
Mshitakiwa alichagua kulipa faini badala ya kwenda jela kutumikia kifungo hicho.
Chanzo: Nipashe