Ni jambo la kusikitisha sana kwamba wagombea wengi wa CCM inapoonekana wamepata kura chache kuliko mgombea wa chama kingine, wanakataa kusign form za matokeo.
Kabla ya uchaguzi huu viongozi, wakiwepo hata JWTZ, walituasa tukubali matokeo. Sasa inaonekana ni pale CCM inaposhinda tu, matokeo yanatangazwa bila mbinde.
Kutokutangaza matokeo wakati wake, kunaleta tension, na vijana wanapodhani kuna mbinu za kuchakachua ili matokeo yaridhishe chama fulani, wanaanza fujo. Tanzania tuna sifa ya kuwa taifa la amani, na nasihi kila mwananchi ajiepushe na tabia inayoweza kusababisha vurugu ambazo sitasababisha umwagaji wa damu au maumivu yasiyo na sababu za msingi.
Maamuzi ya kidemokrasia, hasa pale wananchi wanapoamua kwa uhuru wao kamili kwamba wataongozwa na nani, ndiyo yanayoleta maendeleo ya kuridhisha. Itasikitisha sana kama baada ya miaka hii ya amani na utulivu, tutaanza kuweka doa katika historia yetu, eti fulani na fulani wamepoteza maisha yao katika harakati za kupigania demokrasia ya kweli.