Elections 2010 MUSOMA MJINI kwalipuka: Mwana CCM auliwa!

Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,445
2,268
Wakati wana CHADEMA wanashangilia ushindi wa mbunge mpya Vincent Kiboko Nyerere kwenye viwanja vya wazi, mwananchi mwenye mavazi ya CCM alikatisha uwanjani na kujaribu kuharibu sherehe. Amepigwa panga la kichwa na mwili wake unahifadhiwa hospitali ya mkoa.

(Huko Kisesa Mwanza, wananchi wenye hasira waliochoka urasimu wa kusubiri kutangaziwa matokeo wamechoma maboxi 6 ya kura. Wasimamizi wamekimbizwa. Uchaguzi huenda ukarudiwa.)
 
Wakuu, kinachotokea hapa ni CCM kwa makusudi mazima wanazuia matokeo wakijua kwamba siasa is about ushabiki. Na ushaiki unaendana na hasira, sasa kinachotokea mwz na Atown ni kwamba, watu wataanza mapambano na polisi na umwagaji damu utatokea, then watasema si tulisema?

Swali ni kwamba: Kwa nini wakurugenzi wa halimashauri na manispaa hawatangazi matokeo? hawana calculator ya kujumlisha?
 
JK kama ana akili atuachie nchi yetu ikiwa salama vinginevyo atajikuta tunamkabidhi HAGUE kule aliko Charles Taylor yaani kwenye ICC..........................
 
Jamani waachie nchi yetu tujitawale alaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa CHADEMA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
 
Mafisadi jamani watatumaliza. Tangazeni matokeo. Mnasubiri nini?

Ni jambo la kusikitisha sana kwamba wagombea wengi wa CCM inapoonekana wamepata kura chache kuliko mgombea wa chama kingine, wanakataa kusign form za matokeo.

Kabla ya uchaguzi huu viongozi, wakiwepo hata JWTZ, walituasa tukubali matokeo. Sasa inaonekana ni pale CCM inaposhinda tu, matokeo yanatangazwa bila mbinde.

Kutokutangaza matokeo wakati wake, kunaleta tension, na vijana wanapodhani kuna mbinu za kuchakachua ili matokeo yaridhishe chama fulani, wanaanza fujo. Tanzania tuna sifa ya kuwa taifa la amani, na nasihi kila mwananchi ajiepushe na tabia inayoweza kusababisha vurugu ambazo sitasababisha umwagaji wa damu au maumivu yasiyo na sababu za msingi.

Maamuzi ya kidemokrasia, hasa pale wananchi wanapoamua kwa uhuru wao kamili kwamba wataongozwa na nani, ndiyo yanayoleta maendeleo ya kuridhisha. Itasikitisha sana kama baada ya miaka hii ya amani na utulivu, tutaanza kuweka doa katika historia yetu, eti fulani na fulani wamepoteza maisha yao katika harakati za kupigania demokrasia ya kweli.
 
Inasikitisha na kuogopesha sana
 
Siku zote mroho wa madaraka huwa hana huruma na maisha ya anaowatawala. JK anaona haya kuwa ni yeye pekee ndiye aliyeshindwa kutawala kwa mihula miwili, hapo nafasi ya democrasia ya kweli iko wapi? Au ni maneno tu ya mdomoni?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom