Music library ya rtd(tbc) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Music library ya rtd(tbc)

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by paesulta, Nov 18, 2009.

 1. paesulta

  paesulta JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2009
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35

  Leo ni siku ambayo Wagiriki wanakumbuka miaka iliyopita jinsi wanafunzi wa vyuo vikuu walivyosimama kidete kuondoa Majunta na serikali yao ya kikandamizi hapa Ugiriki.Kulikuwa na kipindi fulani katika TV ya Taifa ambacho walikuwa wanapitia music library yake na kuangalia miziki iliyopigwa marufuku na serikali ya Majunta,na pia katuni na vitu kama hivyo.
  Hii ikanikumbusha sana Redio yetu ya Taifa RTD(sasa TBC).nakumbuka nikiwa mdogo tulikuwa tunasikia wimbo fulani kwa kipindi kifupi na baadae mnapata taarifa kuwa wimbo huo umepigwa marufuku na serikali kurushwa hewani kwa sababu umekiuka either maadili ya ''kiutamaduni'' au ya ''kisiasa''.Kwa namna yeyote,najua kuwa ni nyimbo nyingi sana zilikuwa zinakataliwa kupigwa hewani kwa sababu moja au nyingine.
  sasa kwa kuwa RTD ndio ilikuwa redio pekee wakati huo na studio vilevile za kurekodia nyimbo mpya watakuwa na libraly tajiri sana ambayo imejaa sio tu nyimbo zilizokubaliwa bali hata zile ambazo zilipigwa marufuku.kuna siku kweli tunaweza kuja kuzisikiliza nyimbo hizi kwa kuwa naamini kuwa tupo katika wakati mwingine kabisa tofauti,wakati wa kidemokrasia na ni wakati ambao tunaweza kuangalia yaliyopita kama funzo la tulipo na kule tunakokwenda.Kidogo siku za karibuni nimeona kidogo mabadiliko katika magazeti ya serikali ya Daily News hasa kupitia mtandao ambapo wanajitahidi sana kuandika habari zote bila kuchuja zinatoka katika chama fulani,kitu amabacho ni alama nzuri sana.nadhani ni wakati mahususi kwa TBC pia kuinamia katika upande huo.Wana maktaba ambayo inajisheheni hasa katika swala zima la muziki wa kitanzania,maktaba ambayo kwa kuwa ni mali ya Watanzania wote basi kuna haja ya kuwezesha kazi zilizohifadhiwa humo zinafaidiwa na Watanzania wote.
  mi ni mpenzi sana wa muziki wa dansi kama ulivyokuwa ukiitwa.kuna uhaba sana wa mziki wa dansi ambao tulikuwa tukisikiliza wakati wa miaka ya 80,wa kina Vijana Jazz na Mzee Maneth,wa kina Mlimani Park na wengine wengi.fulsa pekee ya kusikiliza mziki huo kwa sasa ni pale tu ambapo utakuta band music za sasa zitajaribu kupiga tena miziki hiyo ambapo mara zote hawapigi kwa ubora ambao miziki hio ilipigwa originally.
  Basi imefika wakati TBC waachie kazi ambazo zilifanywa na wanamuziki wetu wapendwa wa zamani ziweze kusikika kwa watanzania wote kwa namna ambayo miziki hiyo ilikuwa wakati huo,kwani TBC kuwa mali ya UMMA inamaanisha kuwa kazi zilizofanywa wakati wa RTD ni za UMMA.wasije na kisingizio kuwa wana hati miliki,hati miliki hii ni ya WATANZANIA.
  Naomba kuwakilisha.
   
 2. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Nimekumbuka mbali sana wakati nikiwa field hapo miaka ya mwanzoni mwa 1990's. Mkuu wa maktaba hio pale RTD Pugu rd alikuwa Mama Tatu Mbotoni, nimewakumbuka watangazaji akina Edda Sanga, Mama Sara Dumba, Mshindo mkeyenge, mtaalamu wa studio 3 Bw katembo na wengine engi.

  Sijaasahau mafundi mitambo etu akina Mzee Edmund Mria, Ali said Tunku, Noel Namaloe na wengine.

  Mkuu wetu wote alikua david wakati na SS Mkamba
   
Loading...