Oh, hivi mwanasiasa hawezi kuwa Msomi?
Fundi Mchundo
Pengine kweli ni mgeni katika huu ukumbi au umebadili jina ulikuwepo kwa muda mrefu au ulikuwa msomaji tu. Sina sababu ya kumtukana mtu yoyote tena ambaye simjui lakini kitu ambacho utakutana nacho kwenye forums ni kukubaliana kutokubaliana au vinginevyo.
Kuna mada nyingi sana katika forum hii na huwezi kupata jibu kwenye thread moja na kufikiria umepata majibu unayoyategemea katika nyanja mbalimbali.
Tanzanians tumeezidi na ubabaishaji. WE HAVE DECIDED TO DELEGATE OUR RIGHT TO BE AT THE BATTLE FRONT TO DEMAND AND DEFEND OUR RIGHTS! HAKUNA MTU WA KUKUPIGANIA NI WEWE. SIO LOWASSA WALA JK! Haiwezekani tukawa na huu mtizamo na tukajidanganya kwamba tutaendelea. watu wako majuu, hawafikirii kwamba hiyo majuu ilitafutwa! Au unafikiri huko wasomi wetu wanakothaminiwa walizaliwa wakiwa wanathaminiwa? Its a process na huo uhuru na freedom watu mnayoienjoy huko mliko, kuna watu walipigana kiume mpaka wakaupata huo uhuru ingawa hawakuufaidi. Talk of Martin Luther King NA HAKI ZA WEUSI USA! Leo mtu mweusi anatembea kuifua mbele USA. lakini hajiulizi ni kiasi gani cha gharama watu walilipa kusudi mtu mweusi akombolewe! wengine walifungwa magerezani miaka mingi, wengine walikufa vifo vibaya, kikubwa ni kwamba walikuwa wanahangaikia kitu ambacho walikiamni na leo wewe na yule ndo mko proud kusema kwamba mnathaminiwa huko mliko! Ingawa aliyepigana na kulipa gharama, hakufaidi chochote!
Jamani kuendesha nchi sio kuendesha kampuni binafsi you need the art of compromise! JK cant do each and everything on his own, sasa kama wenye mawazo mazuri mnaogopa kuyatoa eti mtalalamikiwa na system, harafu bado tunalaumu. You will know the pain f the system ukiijoin na wala sio kuwa outsider critique! wasomi inabidi tutumie elimu yetu kuyabadilisha mazingira. hakuna anayeweza kutubadilishia haya mazingira!
Wangapi hapo mko tayari kuacha maisha ya ulaya na kurudi bongo? Kisa eti mazingira duni! Get life!
Muungwana hapo juu kanena na mimi nasema, wasomi ndo tunairudisha nyuma Africa! WE WANT GOOD THINGS BUT WE ARE NOT PREPARED TO PAY THE ULTIMATE PRICE!
Kama jamaa alivyosema, wasomi tutazidi kupokezana vijiti vya ufisadi kwa sababu tunataka kuishi peponi wakati hatutaki kuilipia hiyo pepo kwa gharama stahili! Usitegemee babu au mjomba wangu wa Kwimba apambane na Lowassa wakati mimi mwenye elimu kama Lowassa nimekimbia uwanja wa mapambano. Mi ndo mwenye hoja, common man anakuangalia wewe MSOMI! sasa ukikimbia yeye atafanya nini?
Hapo ndipo dugu yangu BUBU nashindwa kumuelewa maana wanasiasa ndio walio hudhuria madarasa .
USOMI WA WATANZANIA UNAUWALAKINI MKUBWA
unajua kuna kupita darasani na usielimike vilevile kama wengi tulivyo ndio maana nikakutolea mfano SHABAN ROBERT alikomea darasa la saba lakini alikuwa ameelimika vya kutosha.
mimi ningeshauri MFUMO WA ELIMU UTAZAMWE UPYA maana inaonekana mtu anayejua kukariri vizuri ndiye msomi ndugu yangu BUBU usomi ni IQ ILIYO KICHWANI.
NA nchi bila kuwa na wasomi wa kweli kamwe haiwezi kuendelea na ndicho kinachoendelea leo hii TZ.
Bubu! Mengi unayosema nakubaliana nayo. Tatizo ni huku kudai remuneration pekee ndio tiba ya matatizo yetu. Bila kuwa na mazingira mazuri ya kazi, uwajibikaji na naam, kuthamini na kutumia kwa busara rasilimali yetu (natural na human) hatutafika mbali. Hao unaowaita mafisadi wanalipwa vizuri sana ( wengine walikuwa nje na kurudi nchini ati kutumikia taifa) na wamesoma vizuri lakini wote wana hili tatizo la "sense of entitlement" bila kuwa na uchungu wa taifa letu. Kwa vile unakataa kuwaita wanasiasa wasomi,basi tupe definition yako ya usomi.
Kama nilvyosema,Bubu, mengine nakubaliana na wewe , mengine sikubaliani. Daktari kushindwa kuongoza wizara ya fedha si kwa sababu hajui dr au cr, ni kwa sababu ana walakin katika uongozi. Kiongozi ni yule mwenye upeo (vision) na anayeweza kuwavuta wanaomfuata kuamini katika vision hiyo. Kiongozi (bora) ni yule anayeangalia na kutambua nguvu na udhaifu wa wale anaowaongoza na akautumia ipasavyo. Kiongozi(bora) ni yule anayetambua limits au udhaifu wake na kuukabili ipasavyo. Katika hali hiyo, anakubali kukosolewa na kuomba ushauri pale inapobidi. Kama hajui dr au cr, anahakikisha anapata mtu anayejua hizo na kumtumia kikamilifu. Kiongozi (bora) hatasita kuwaambia anaowaongoza ukweli wa hali halisi na kuchukua hatua zinazotakiwa hata kama zitakuwa na hasara kwake binafsi. Kwa maneno mengine, si populist!Kiongozi(bora)anaongoza kwa mfano-kama kujibana mikanda, wote tunajibana. Kiongozi bora anawaheshimu anaowaongoza akitambua hao ndio watakaomletea yeye mafanikio. Kiongozi si lazima awe msomi au mtaalam. Kwa mfano; Yesu Kristu, mtoto wa fundi seremala, Mtume Mohamed S.A.W hakwenda shule, Buddha mtoto wa mfalme aliyedekezwa kabla ya kuamua kuondoka na kwenda kutafuta ukweli, Malcolm X alikuwa pimp,drug dealer,convict; akajibadilisha na kuongoza mapambano ya kudai haki ya wetu weusi nchini Marekani, Bill Gates-college drop out n.k. Kiongozi anaweza kuwa msomi, kwa mfano Waziri Mkuu wa kwanza wa Singapore Lee, ameliongoza taifa lake kutoka kwenye umaskini hadi hapo walipo sasa. Viongozi bora wa kiafrika ni wakina Lumumba, Mandela ( aliyeongoza taifa lake kusameheana,utakumbuka alikubali kuitwa mahakami kama raia mwingine na hakujiona Mungu mtu), Nyerere (pamoja na madhaifu aliyokuwa nayo, hakuna mtu aliweza kudoubt integrity yake na pale alipoona mambo yamemzidi alimpisha mwingine),Thomas Sankara (aliwaongoza wa Bukinabe kwa mifano ;k.m. alikataa kununuliwa gari la kifahari na kuendelea kutumia VW aliyokuwa kiiendesha kabla ya kuwa mtawala), Castro, Mahatma Ghandhi, na wengine zaidi. Uongozi si unyapara kama tunavyodhani. Kukaripia tuu,kufokea, kudhalilishana peke yake si uongozi bora. Unahitaji ku'motivate' hao unaowaongoza.
Ukiwa na kiongozi bora utafanya kazi kwa bidii zote kwa vile unajua yuko pamoja nawe.
Naona niishie hapa maana nimeshaongea mno!!