Museven hata wewe?

Kwenye siasa hakuna rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu. Wahenga wakisema tenda wema benda zako.... so ingekuwa kusubiri shukurani basi ni mataifa machache sn ambayo yasingeishukuru tz..,...
 

dawa yenu inachemka, mungu alishawalaani suku nyingi.
 

Kuliko kumfadhili mwanadamu mfadhili mbuzi utamla nyama!
 
Ndio maana wazungu hawapigani vita za kijinga wala kuunga mkono viongozi bila kwanza kuangalia maslahi yao ni nini. Ukiona wameanza vita jua kuna mafuta, gesi au wanamlinda yule ndugu yao wa damu aliyepo wa mashariki ya kati. Hujawahi kujiuliza inakuwaje Saudi Arabia inayoongozwa kifalme na ambayo haina uchaguzi wa kidemokrasia na hata wanawake hawapigi kura ni mshirika mkubwa wa Marekani wakati Iran yenye uchaguzi wa kidemokrasia ni adui namba moja wa hawa jamaa? Mbona hatuoni mzungu Mogadishu akipambana kuwaokoa wananchi wa kule?

Nchi na wanasiasa wakubwa huwa wana maslahi ya kudumu na sio marafiki wa kudumu. Ndio maana Sadam Hussein aliyekuwa kipenzi wa nchi za magharibi huko nyuma aligeukwa na kubamizwa pale alipoonekana kwenda kinyume na maslahi yao hasa pale alipodhani kuwa anaweza kuingia kuwait tu na kuchukua visima vya wakubwa halafu wamwangalie tu.
 

huwezi kutoka chumbani kwako ukaenda sebuleni kwako halafu ukasema umeenda kutembea kwa jilani huko ni kujidanganya.
 
Babu M7 anaona mna muwekea usiku tu wakati umri umekimbia na yeye anataka kua Rais mteule wa E.A Federation, kampata na mwenzie mwenye ndoto kama zake PK itakua kaahidiwa umakamu wa Rais and if possibly Urais wa E.A, Uhuru nae akaona hapa atapiga bingo ndefu akijiunga nao, basi wamekutana wenye Interest zinazoendeana waache waende alaaa!!!
 

wakuu kwakweli inasikitisha sana kwa jinsi nchi yetu ilivyotengwa na kudharauliwa kiasi hiki. Lakini mimi ninafikiri kuwa hakuna jambo linalotokea pasipo sababu maaalumu. huwezi kujua mungu anatuepusha na kutupangia nini huko mbele, labda ndio njia pekee kabisa ya sisi kujifunza na kuacha utaratibu wetu wa sasa wa kutotunza rasilimali za taifa na kuwaachia wageni wakichuma uchumi wetu na sisi tukiwa busy kuuza madawa ya kulevya. Hakika kutengwa huku kutatufanya tuwe watu wamoja na tutafuta njia nyngine za kuimarisha uchumi wetu. Tanzania tuna kila rasilimali ni suala la uongozi tu na matumizi yasiyo ya lazima ya serikali yetu. \
dhambi hii ya kujitenga maadamu si sisi tuliowatenga hakika sisi tutabaki salama ila wao hiyo dhambi itawatafuna tu
 
Kwanini kuandikia mate na wino upooo!! Tanzania imecheza role yake, siku zote taifa letu huwa wa kwanza kujitolea na huu utamaduni sii geni humu. ukweli kila mtazamo hua una gharama yake. La msingi na muhimu ni kujitosheleza na kujipanga humu nchini ili tuUkuze uchumi wetu na tujikimuu ndani soko letu, kwani idadi ya 45million ni mzigo tosha kwa taifa. Siasa yetu nyeti "Nyumbani kwanza" Majirani baadayeee.
Together we stand.
 

Watanzania tunajihujumu wenyewe - Kiswahili mingi (porojo), vitendo kidogo vilivyoambatana na uswahiliuswahili. Hata Baba wa Taifa angekuwa hai leo hii asingefurahishwa na uswahili huu uliopitiliza. Sasa bahati iliyoje, tumepata punda wa kumtwisha mzigo wetu (mwendelezo wa uswahili)!!!!
 
Usilalamike sana kijana, hao wanaoitenga tz watakuja wenyewe na wataipigia magoti tz kwani hata wakisema waungane tz ndo nguzo yao. Kwa mfano burundi wanalishwa na tz, rwanda inategemea shamba lao lililopo kongo ambalo tz imelifunga lisitumiwe na rwanda. Uganda naye waasi wamemzidi nguvu hivyo bila msaada toka tz nchi mda si mrefu itakuwa mikonon mwa waasi, kenya nao soko lao kuu la bidhaa zao zaidi ya asilimia 60 lipo tz. Tz hatuna cha kupoteza kwa kutengwa na hao wauaji ambao kesi zipo zinaunguruma
 

Huko kote kwenye uchumi usidhani akili yake ipo huko. Anachotaka ni fast tracking ya political federation ili awe rais wa kwanza wa EAC. Ameishayasema mwenyewe mara kadhaa. Bila shaka atakuwa rais wa Uganda, Kenya na Rwanda. Burundi sina uhakika kama wanakubali wazo lake. Kama Kenya wataona wanapata manufaa kiuchumi bila shaka watakubali jamaa awe kama mfalme pasipo na faida yoyote kwa nchi.

Hadi mwaka 2018 ambapo wanadai reli yao itakuwa tayari, mengi yatakuwa yametokea hapo katikati.
La kwanza, je Museveni atafanikisha kumpa urais mwanaye au itabidi yeye mwenyewe aendelee. Tayari akina Tinyefunza wameisha ikimbia Uganda na inaelekea mambo si shwari sana jeshini Uganda.
La pili, je Kagame atabadili katiba ili aendelee kutawala Rwanda? Kwa katiba ya sasa inabidi ampishe mtu mwingine. Akifanikiwa kubadili katiba, wanyarwanda wengine watakuwa kimya tu?
Sipendi kutabiri lakini pia siamini kama viongozi wote hao wawili watakuwa madarakani mwaka 2018. Kama kutakuwa na mabadiliko ya uongozi, hao/huyo atayefuata/watakaofuta, wataendeleza hatua za sasa? Muda ni mwalimu mkuu wa mambo yote, tusubiri.
 

Mkuu kama Marehemu baba wa taifa angekuwepo haya anayoyafanya Museven, Kagame na Kenyata sidhani kama yangetokea kumbuka Nyerere alikuwa anakemea yote maovu yanayofanywa na viongozi wa nchi hii kwa hiyo huu mpasuko usingetokea. Tatizo hapa ni mtafaruku kati ya Kikwete na hawa viongozi wenzake na sio mtafaruku wa Tanzania na hizi nchi. na kumbuka Nyerere angekuwa hai sidhani kama Kikwete angekuwa Rais wa nchi hii Kifo cha Nyerere ni mipango yao na hapa tulipofika wametufikisha kwa makusudi yao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…