Pesa yoyote yenye kuheshimika duniani na kukubaliwa huwezi kuhangaika mpaka kwa wenyeji kukusaidia kubadili.
Mimi Riyal zangu Bangkok nilihangaika nazo sehemu nne bila mafanikio. Sikatai kuwa kuna sehemu zinaweza kukubalika pengine, lakini niliambiwa na jamaa wa Bureau ya Bangkok kuwa hawazitaki.
Mbona nabadili Yen ya Japan bila tatizo kokote?
Mimi si mgeni wa safari, Sheikh. Nafahamu kuwa watu wa Oman na Saudi Arabia wanapapenda sana Thailand, hasa kwa ajili ya matibabu na starehe.
Kuna Arab Town Bangkok , ipo Mtaa wa Sukhumvit Soi 3, au kwa treni ni Nana station.
Unakula Sheesh Kabab za Iraq, lakini kwa bahati mbaya ni sehemu ya umalaya, hasa wa kutoka Afrika.
Na haya ndiyo mambo rasmi wageni wengi wanafuata Pattaya.
Muuzaji na Mnunuzi.