Wakati huo tukiwa na bikira za akili na maarifa,wakati wa utakaso...watoto Tanzania nzima tukiwa kitu kimoja ktk umoja wa Taaluma na michezo,tukiunganishwa ktk umoja na upendo na mashindano ya UMITASHUMTA na UMISETA,Wakati haupo tena upande wa watoto wetu.
Elimu ilikuwa sawa,mitaala yenye kufanana iliyotujaza maarifa na uweledi,hadithi nzuri ktk vitabu zilizotufundisha jinsi ya kuheshimu wakubwa,walimu na wazazi wetu.Vitabu vyenye simulizi ya kukemea uwizi,ulafi na uchoyo..haya ndiyo mambo ya kina CHOPEKO NA MNOFU,ADILI NA NDUGUZE,PAZI NA JOGOO,SHUJAA SETH BENJAMIN
Tuliokuwa watoto wa wazazi ambao ni watumishi wa umma tulihamahama huku na kule,kila tulipoenda tulikuta ufanano wa kilichofundishwa,lakini leo mambo ni tofauti...anachokisoma mtoto wa darasa la tano Mjimwema Primary school si sawa na anachosoma mtoto wa Tusiime ya pale Tabata.
Nini kimetokea ktk elimu yetu???
nikiwaona Juma na Roza inanikumbusha mbaliiii sana.