Muono wangu wa mechi

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
NILIYOYAONA WHITE HART LANE

Tottenham 3-0 Manchester United

1. Timu inayotaka ubingwa ndiyo hucheza hivi, Spurs leo wameonyesha kwanini wanatajwa kwenye mbio za Ubingwa, kuanzia kwenye kukaba mpaka kushambulia vijana wa Pochettino walikuwa bora hasa kipindi cha pili. Ukiutaka ubingwa hunabudi kuutafuta na ndicho wanachokifanya Spurs.

2. Achana na Eriksen, Lamela, Alli na Kane, nyuma ya hawa kuna "wabeba maji" wawili Dier na Dembele, washikaji hawa wawili ndiyo wanoleta uwiano wa kukaba na kushambulia ndani ya Spurs ukiona Eriksen na Alli wanang'ara basi ujue nyuma yao kuna hawa.

3. Kama huko kwenu kuna Coutinho ama KDB ama Wllian basi huku kwetu pia kuna Christian Eriksen, mshikaji kutoka Scandinavia mpira unamtii na kumheshimu haswa, anaupeleka anakotaka na mpira unaenda unakopelekwa, fundi wa kidenish huyu.

4. Kwasasa duniani Marcelo ni moja ya mabeki wa kushoto bora kabisa, kila nikimwangalia Danny Rose ni kama naona kiasi ubora wa Marcelo ndani yake hasa kwa namna alivyokuwa anashambulia. Ana kasi, anapiga krosi na "foot work" yake ni nzuri.

5. Kuna Manchester United halafu na kuna De Gea, kwasasa inaonekana kama United ndiyo wako ndani ya De Gea na sio kinyume chake, De Gea mpaka sasa ndiye anayeamua matokeo mazuri ya United na ndiye mchezaji mwenye "consistence" zaidi chini ya LVG.

6. Luis Van Gaal naomba majibu hivi ulipomtoa Rashford na kumwingiza Young ulitaka nini kitokee kwenye eneo la mbele la United? Kwasababu baada ya kutoka kwa huyu dogo Alderweireld na Vertonghen walipumzika na hapo ndipo zahama ikahamia upande wa pili.

7. Fosu-Mensah dah, toka alipoumia na kutoka dakika ya 68 na kuingia Darmian basi hapo ndipo uwanja ulipoinama na magoli yote matatu yakatokea upande huo huo, dogo aliupiga mpira mwingi sana leo.

8. Carrick na Schneiderlin ni "combination" ambayo haikuweza kuwazuia Spurs kutawala eneo la katikati, unaweza kusema eneo la katikati la United lilikuwa ni kama baiskeli ambayo mbele ina gurudumu la mbao na nyuma ina gurudumu la kawaida na kinyume chake.

9. Memphis Depay kumbe bado yupo! Bishoo wa kidachi huyu leo atakuwa alionekana na wengi kwasababu ya tukio la kugombana na Walker TU. Leo amecheza dakika 18 sio mbaya hasa ukizingatia kwamba mpaka sasa haijui kesho yake.

10. Sio mbaya kwenye vijiwe mbalimbali vya drafti, bao, pool na michezo ya kubashiri mashabiki wa Manchester United mkaendelea kumzungumzia Jose Mourinho na umahiri wake.

NB: Mchezo ulichelewa kuanza kwa dk 30 kwasababu klabu ya Manchester United ilikumbwa na matatizo ya "jam" ya magari kwa masaa mawili na kufika uwanjani dk 17 kabla ya muda wa mechi kuanza..............!!!!!!
 
Back
Top Bottom