Muongozo: Programming Language

Amina mkuu! na ubalikiwe katika mishe zako... pamoja tutafika!
 
Reverse engineering inalipa kweli kwa bongo hii?! Huwa kuna vipaji vingi tu vya programming kwenye nchi maskini vinakufa au kupotea kwa sababu hakuna pa kufanyia kazi! Labda kwa wenzetu ambako kuna programming firms za maana.
tatizo sio programming firms! tatizo waafrika tunapenda kuajiliwa sana alafu vilevile mara nyingi tunapopata fulsa kama hizi za forums za kuwafikia wakuu unakuta tunaongelea mambo yakuharibu, yasiyo na umuhimu kwetu! mara ooh sijuwi JPM nini sijuwi nini badala ya kumsogelea na kumpa deal za kuinvest na kuendeleza nchi badala yake unakuta tumejikita kwenye siasa sijuwi nani kafungwa nani kaachiliwa ilimradi tupige kelele tu bila hata ya kujuwa kafungiwa nini! atajuwaje kama yuko na wataalamu wa mambo fulani? ndio maana unaona wanakimbilia kwenda kutuletea wachina! huku kwetu Rwanda baada ya kugundua siri ya urembo, hivi kila siku tunampigia hodi mzee wetu, ndio maana unaona hata campaign ya MADE IN RWANDA imeshika hatamu na Mungu akijalia watu watakuwa wanakuja huku kununuwa vifaa, kama vile tumashine twa cofee, ice cream, mashine za michezo ya watoto(fair) na nyinginezo au angalau hata system za umwagiliaji, jamani tuna safari ndefu! tupunguze siasa zinatuumiza wabunifu!
 
Mkuu nimependa maelezo yako! Ila kumbuka na njaa yetu inatufanya tupoteze hata hobby zetu tubaki kuishi kwa kuganga njaa!! Imagine graduate katoka chuo maisha mtaani magumu atawaza vipi kufanya vitu vya hobby yake?! Wengi wako radhi hata kwenda kufanya kazi excel tu ili mradi anapata kimshahara...
 
mkuu nazani C ndio nzuri kama ni high level plz kama una material nifanyie mpango hata kama kutakuwa na chochote kinahitajika nipo tayari kukilipia mkuu.
Ngoja nitacheck kwenye library zangu, ingawa nikiri tu kuwa sijawahi kufanya programming kwenye microcontrollers kwa kutumia C, nimefanya fanya kwa kutumia assembly language
 
Mkuu wewe potential sana!!
 
1. Wewe si ndio umeniita lakini?
2. Halafu uwe na adabu, dada yenu kitchen party tayari, nasubiria kuweka ndani very soon. Ndo nishakuwa shemeji yenu muwe na adabu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…