Muongozo: Programming Language

Automobile hizo zina involve sana C++, C, na assembly.
unaweza anza na C.
mkuu unaweza ukanisaidia kupata basic ya hiyo C++ ili nifaham ni kitu gani maana mm ni mweupe kabisa
 
ha! vipi ndugu yangu? kumbe kunamajukwaa ya vitu vya kueleweka? mi kazi kumkomalia yule Interahamwe jMali wakati kuna mada za kujenga jamii! Dah nilikuwa nimepotea kabisa anyway wacha nirudi kwenye mada, unajuwa kama hauelewi mambo some guys can confuse you mate! nakumbuka kipindi bado nipo darasani mwalimu wangu mmoja wa kijerumani alikuwa ananing'ang'anizia C++ kwenda kiwandani hata sikukutana nayo aisee yani kazi ilikuwa ni kudesign na kuprogram kwa kutumia Ladder Logic na Function Block diagrams for PLC's baasi yani hadi najuta kwa nini nilikuwa na attend hata somo lake! kwangu hivi ni kumsikiliza mteja, kutengeneza algorithm na kufyatua, mchezo kwisha! NB kwa wale wanaosomea Electrical Engineering ningewashauli wasipoteze mda wao kwenye lugha yoyote ile kwani Ladder Logic ni rahisi na inaendana na taaluma ya umeme
 
mkuu mm ni fundi umeme wa magari so nahitaji sana kujifunza hayo makitu kwa kuongeza zaidi ujuzi wangu sababu kuna kazi nyingi sana zinahitaji kuprogram sasa hivi kwa haya magari ya kisasa.
je ni kipi natakiwa kuanza nacho sababu nimweupe kabisa
labda naweza kukusaidia! kwani ni matatizo gani uliyokutana nayo hadi uhitaji kujifunza programming? gari zote huwa programmed tayari vile vile kuna diagnosis tools ambazo ziko tayari kukurahisihiha kazi na kama unahitaji kureprogram then unaweza ukapata a specific software for a car you are trying to fix, hope this helps...
 
mkuu ni hivi huwa napenda sana kufaham kiundani how car ecu communicate and work.mfano diagnosis mashine ni vipi inawasiliana na gari ni vipi ina communicate na gari na kutambua problem ya gari??

mfano kwenye millage change kuna mashine hufanya kazi hiyo ww unacconect kwenye gari au unatoa eeprom kwenye cluster na kusoma data zake na kuzichange kwa mashine but mm nilikuwa najifunza kile kinachofanywa na mashine mahesabu ya hexdecimal.

then kuna kitu kama immobilizer jinsi ya kuprogram bongo ss mafundi wana copy na kupaste lkn mm nilipenda niweze kuandika data mwenyewe kwenye chip\eeprom mwanzo mwisho na mpaka code zakuweka kwenye funguo niziandike mm.


magari ya sasa hivi yanatumia CAN =COMMUNICATION AREA NETWORK imakuwa ni taabu sana sio kama zamani gari inakuwa na waya 300 siku hizi waya 5 tuu zinafanya kazi zaidi ya 20 .

mkuu nazani utakuwa umenielewa plz kama unaweza kunisaidia
 


salaam kwako Mkuu! Diagnosis tool(OBD 2)zipo nyingi tu za tofauti kuna makampuni mengi yanayotengeneza na kuuza online na huwa zinatofautiana kwa ubora wake, wapo wale wanaotengeneza software ambayo unatia kwenye laptop yako na kucommunicate na gari lako kwa njia ya wireless kupitia OBD2 port au wale wanaotengeneza machine kabisa kwa dhumuni hilo, eitherway they do exactly the same job! cha muhimu ni kujuwa functions na interpretation but believe me ni kitu rahisi sana kwa sababu hakuna kitu cha ajabu utakacho fanya zaidi ya kupokea signals kutoka kwenye ECU, ECU ndio ubongo wa gari with I/O conections inapokea informations kutoka kwenye sensors then kuchukuwa maamuzi kutokana na program iliyoandikwa na designer mwenyewe then send a command through the output pins ni hayo tu! vilevile kama unataka kujuwa Kuhusu ECU tuning, kuna tutorials kibao online, nenda kwenye google uandike ECU chip tuning au ECU programming, na kama unataka kufanya practices kuna software za kukusaidia kama vile ku tune vehicle performance or change the way it behaves.
cha kwanza kabisa ni kutafuta Tuner ambayo inaweza ku support the model of your car na mwaka ilipoundwa, tuner is what will extract the cars data to your computer as a file then you can edit this file inside an editor make changes and upload the file back to a car using the tuner, ila Kusudi ufanikiwe, unahitaji vitu viwili vya muhimu

1) Software, It may be overwhelming at first using it and it is! lakini ukikaza msuli baada ya mda fulani utaelewa tu, basically all you are doing is changing the numbers that correspond with different behaviors within the car, kwa mfano, Torque has number 1-255 On your car, inaweza ikawa imesetiwa kwenye 200 lakini wewe vilevile unaweza ukaiongeza kama ukipenda, kitu kingine kama ulivyosema, tuning requires HEX editing skills, this is the reality, lazima uwe na huo ujuzi kusudi ufanikiwe, lakini vilevile there are many online resources that will teach you about HEX, kwa hiyo ukitaka kufanikisha kazi yako basi lazima uwe na vifaa pamoja na uelewa

2) Tuner Kit, hii inahitajika because its purpose, to download/upload cars map file to your computer, tuner zipo nyingi tu tofauti zipo za malaki na za maelfu lakini kiukweli zote zinafanya kazi sawa cha muhimu ni kupata inayoingiliana na gari yako, nafikiri umenielewa.
 
mkuu mm nahitaji kujifunza pythoni,HTML and XML nitapataje material na vip nianze na ipi hapo?
 
Kumbe niko juu kweli hata ukidiscuss vingine lazima umkumbuke jmali, hahaha nasikia unataka kutoa Kagame programming language 😀
 
mkuu mm nahitaji kujifunza pythoni,HTML and XML nitapataje material na vip nianze na ipi hapo?
Kwa jinsi ulivyoandika inaelekea huna idea kabisaaa. Ingia youtube au google tafuta kwanza mchepuo unaoutaka halafu ndio uje kwenye chaguzi za lugha.
 
nikitaka kuprogram microchip/microcontroller nisome ip
 
Kumbe niko juu kweli hata ukidiscuss vingine lazima umkumbuke jmali, hahaha nasikia unataka kutoa Kagame programming language 😀
lol! unajuwa we ndugu yangu hovyo sana kiasi cha kunifanya niwe nakuona nuksi! mi naona zile siasa za kuharibu bora uziache tung'ang'anie kwenye kujenga nchi na ujuzi kwa wadogo zetu, italipa!!! kwani hata Raisi wetu ndio jambo linalomkosesha usingizi, trust me! iiif we mean it, even Chinese may end up going back in to their country they are not better than us anyway, tatizo hamjitumi mnashinda mkiwanga kuhusu Kagame na mishe zake za kutufikisha at the mountain top, tabu tupu! NB kumladhi! usilete siasa huku watu wanataka kujiendeleza jMali
 
nikitaka kuprogram microchip/microcontroller nisome ip
You can program in assembly language which or go direct to C which works best for microchip or related microcontrollers like Arduino or 68k Motorola
 
Mkuu fuata ushauri wa mchambawima1! Ila kama unainterest na kuprogram eeprom soma assembly language or kama unataka high level language jifunze C
 
Mkuu fuata ushauri wa mchambawima1! Ila kama unainterest na kuprogram eeprom soma assembly language or kama unataka high level language jifunze C
Hivi mkuu kwanini despite ya kwamba kuna programmers wengi wanaosema wanajua c na assembly tz ila hawako interested na malware and reverse engineering na system programming
 
Kwa jinsi ulivyoandika inaelekea huna idea kabisaaa. Ingia youtube au google tafuta kwanza mchepuo unaoutaka halafu ndio uje kwenye chaguzi za lugha.
hakika hizo language sina aideal nazo but naijua c++
 
Hivi mkuu kwanini despite ya kwamba kuna programmers wengi wanaosema wanajua c na assembly tz ila hawako interested na malware and reverse engineering na system programming
Reverse engineering inalipa kweli kwa bongo hii?! Huwa kuna vipaji vingi tu vya programming kwenye nchi maskini vinakufa au kupotea kwa sababu hakuna pa kufanyia kazi! Labda kwa wenzetu ambako kuna programming firms za maana.
 
SHUKRANI SANA MKUU yaani sijui hata nikwambiaje uliyo yaandika hapo ndio haswaa lengo langu mkuu yaani ungejifanya ni mtabili basi leo ungenibamba sana mkuu.nashukuru sana kwa kunielewa then na kwakunipa ushauri.napenda sana hayo uliyoyasema coz kuna faida nyingi sana kuna magari mrngi sana bongo yanakufa na kupaki wakati solution yake ni ndogo sana kunamagari truck zinazo kuja na mfumo wa ADBLUE zinapark na kufa kisa mafundi or ADBLUE imekwisha wakati kuna option ya kuiremove.

kuna magari kibao yana paki kisa kuna sensor mfano MAF sensor or gari inakuwa na bad pofermance kama ulaji sana wa mafuta kisa EGR imekufa wakati kuna option ya kuremove kwenye ECU.

ulaji wa mafuta kwenye magari bongo imekuwa mzozo wakati ukifanyia ecu programming gari inapunguza.tatizo bongo hatuna vyuo vya uhakika.
mkuu kama huto jali mawasiliano yangu ni 0717228064 naomba unicheki mkuu tuongee na ubarikiwe sana.

soon nitakupa mlejesho ngoja nikusanye kwanza vitendea kazi.mashine zakupimia tuu ninazo za kutosha hilo halina shida.
 
hoj
Reverse engineering inalipa kweli kwa bongo hii?! Huwa kuna vipaji vingi tu vya programming kwenye nchi maskini vinakufa au kupotea kwa sababu hakuna pa kufanyia kazi! Labda kwa wenzetu ambako kuna programming firms za maana.
hoja nzuri mkuu lakini unajua ukifuatilia vzur historia ya mataifa makubwa katika sekta za computing mfano marekani unakutana na fact ya kwamba vitu vilianza kama hobby watu kama wakina Richard stallman walikuwa wana program for the sake of knowledge.Lakini sisi kidogo tumeanza tofauti sisi tumeanza na stage ya ku program kwa ajili ya hela tumeanza stage ambayo wenzetu ndo wapo sasa hvi na maybe ndo sababu kubwa hatuendelei sana kwenye hii sekta kwa sababu kla mtu anaweza hela na kazi passion ni wachache sana
 
Mkuu fuata ushauri wa mchambawima1! Ila kama unainterest na kuprogram eeprom soma assembly language or kama unataka high level language jifunze C
mkuu nazani C ndio nzuri kama ni high level plz kama una material nifanyie mpango hata kama kutakuwa na chochote kinahitajika nipo tayari kukilipia mkuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…