Mungu ndani ya Gereza

Mungu ndani ya Gereza

Sosoma Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2020
Posts
312
Reaction score
281
Mimi ni kijana mkimya niishiye Romani, mwenye umri wa miaka 20 nami ninafurahia kusoma shuhuda binafsi. Mara ya kwanza nilipokutana na Mchungaji Mwadventista, aliniuliza, "Ni aina gani ya vitabu upendavyo kuvisoma?"

Nilimweleza kitabu ambacho nilikisoma mara ya mwisho, ushuhuda binafsi ulioandikwa na mwandishi Mkristo. Wiki moja baadaye, Mchungaji aliniletea vitabu vingi vilivyojawa shuhuda binafsi. Ni shauku yangu siku moja nipate kuandika ushuhuda wangu binafsi.
Kama ningeandika ushuhuda binafsi, ningeanza na kusimulia nyakati za furaha utotoni mwangu. Ningesimulia vile nilivyokuwa ninamchokoza babu na bibi, hata wafikie hatua ya kukasirika. Nilikuwa tu na umri wa miaka 4 au 5, nami nilifurahia mno kuwachokoza.

Kama ningeandika ushuhuda binafsi, ningesimulia siku yangu ya kwanza shuleni. Ilikuwa siku ya furaha. Bibi alinipeleka shuleni na baadaye kunisaidia kufanya mazoezi yangu ya nyumbani. Babu na bibi walinipenda sana. Niliishi pamoja nao hadi nilipoenda gerezani.

Ningeandika ushuhuda binafsi, ningesimulia nyakati za furaha gerezani. Ningesimulia kuhusu watu wema walionitembelea, kama Mchungaji Mwadventista aliyetutembelea mara moja kwa wiki kunifundisha mimi pamoja na wahalifu wenzangu kanuni za maisha na kumcha Mungu. Mchungaji huyo aliwasili pamoja na wanachuo watatu, wakatufundisha wakitumia picha za kurusha ukutani (Powerpoint).

Nilitoroka shule baada ya darasa la nane, hivyo kila hotuba iliyonifundisha lilikuwa jipya na la kuvutia. Baada ya kila hotuba iliyoambatana na picha vielelezo, walitusimulia kisa kutoka katika Biblia. Pia tuliweza kuomba na kuongea pamoja.

Ningeandika ushuhuda binafsi, ningesimulia muda mbaya sana maishani mwangu. Ni kipindi cha miezi tisa tangu nitupwe gerezani nilipokuwa na umri wa miaka 17 ili nitumikie kifungo cha miaka 12. Nilikuwa mpweke kabisa. Hapakuwepo mwana familia ye yote aliyenitembelea. Na wala hakuna aliyetafuta wakili apate kunitetea.

Bibi yangu alikufa miezi kadhaa kabla sijatupwa gerezani, naye babu alikuwa mzee tena mgonjwa hoi. Siku zote nikiwa rumande sikuwahi kusikia neno la upendo. Ila nilipofika gerezani mambo yalibadilika. Baadhi ya askari magereza ni wema, hasa yule mwanamke aliyepewa jukumu la kuniangalia ahakikishe ninapata badiliko la tabia.

Pia ninapenda sana programu ya huduma za magerezani iliyokuwa inaendeshwa na kanisa la Waadventista. Kupitia programu ya kila juma, nimekutana na watu wazuri ajabu tukafahamiana. Sikuwa nimejua naweza kupata watu ambao naweza kujenga urafiki wa karibu jinsi hiyo.

Waadventista huongea kwa upole na upendo, nao wamenifundisha mimi kuishi maisha mema yenye kumtumainia Mungu. Hilo ni muhimu sana kwangu.

Nimekuwepo gerezani kwa miaka mitatu na miezi saba, na miaka miwili ijayo ninaweza kustahili kuwekwa huru niwe uraiani nikitumikia kifungo cha nje. Hilo litawezekana endapo mwenendo wangu utakuwa mzuri. Napenda kudhihirisha kuwa naweza kuaminika na kuwa mtu wa manufaa katika jamii.

Ningeandika ushuhuda binafsi, ningekiri kuwa nimepitia maisha ya huzuni kwa kipindi cha miaka 20. Ni vigumu kwangu kuzungumzia jambo hilo. Familia yangu ilikuwa na matatizo magumu ya kifedha. Hawakuwa karibu nami nilipowahitaji sana kiuchumi. Mambo mengi ya kikatili yamenipata. Hii ndiyo sababu ni mkimya kutokusimulia historia ya maisha yangu.

Iwapo bibi yangu hangalikufa, singaliingia matatizoni hadi kutupwa gerezani. Baada ya kufariki bibi, sikupata malezi sahihi nikawa mkorofi hata kutumbukia kwenye kosa la mauaji.

Baada ya kutoka gerezani, nitapenda kuwa na familia yangu binafsi. Nataka kufanya jambo la manufaa maishani mwangu. Ila kwa sasa mimi ni kijana mkimya nipendaye kusoma shuhuda binafsi.
Asanteni kwa kunisikiliza!!!
 
Mimi ni kijana mkimya niishiye Romani, mwenye umri wa miaka 20 nami ninafurahia kusoma shuhuda binafsi. Mara ya kwanza nilipokutana na Mchungaji Mwadventista, aliniuliza, "Ni aina gani ya vitabu upendavyo kuvisoma?"
Nilimweleza kitabu ambacho nilikisoma mara ya mwisho, ushuhuda binafsi ulioandikwa na mwandishi Mkristo. Wiki moja baadaye, Mchungaji aliniletea vitabu vingi vilivyojawa shuhuda binafsi. Ni shauku yangu siku moja nipate kuandika ushuhuda wangu binafsi.
Kama ningeandika ushuhuda binafsi, ningeanza na kusimulia nyakati za furaha utotoni mwangu. Ningesimulia vile nilivyokuwa ninamchokoza babu na bibi, hata wafikie hatua ya kukasirika. Nilikuwa tu na umri wa miaka 4 au 5, nami nilifurahia mno kuwachokoza.
Kama ningeandika ushuhuda binafsi, ningesimulia siku yangu ya kwanza shuleni. Ilikuwa siku ya furaha. Bibi alinipeleka shuleni na baadaye kunisaidia kufanya mazoezi yangu ya nyumbani. Babu na bibi walinipenda sana. Niliishi pamoja nao hadi nilipoenda gerezani.
Ningeandika ushuhuda binafsi, ningesimulia nyakati za furaha gerezani. Ningesimulia kuhusu watu wema walionitembelea, kama Mchungaji Mwadventista aliyetutembelea mara moja kwa wiki kunifundisha mimi pamoja na wahalifu wenzangu kanuni za maisha na kumcha Mungu. Mchungaji huyo aliwasili pamoja na wanachuo watatu, wakatufundisha wakitumia picha za kurusha ukutani (Powerpoint). Nilitoroka shule baada ya darasa la nane, hivyo kila hotuba iliyonifundisha lilikuwa jipya na la kuvutia. Baada ya kila hotuba iliyoambatana na picha vielelezo, walitusimulia kisa kutoka katika Biblia. Pia tuliweza kuomba na kuongea pamoja.
Ningeandika ushuhuda binafsi, ningesimulia muda mbaya sana maishani mwangu. Ni kipindi cha miezi tisa tangu nitupwe gerezani nilipokuwa na umri wa miaka 17 ili nitumikie kifungo cha miaka 12. Nilikuwa mpweke kabisa. Hapakuwepo mwana familia ye yote aliyenitembelea. Na wala hakuna aliyetafuta wakili apate kunitetea.
Bibi yangu alikufa miezi kadhaa kabla sijatupwa gerezani, naye babu alikuwa mzee tena mgonjwa hoi. Siku zote nikiwa rumande sikuwahi kusikia neno la upendo. Ila nilipofika gerezani mambo yalibadilika. Baadhi ya askari magereza ni wema, hasa yule mwanamke aliyepewa jukumu la kuniangalia ahakikishe ninapata badiliko la tabia.
Pia ninapenda sana programu ya huduma za magerezani iliyokuwa inaendeshwa na kanisa la Waadventista. Kupitia programu ya kila juma, nimekutana na watu wazuri ajabu tukafahamiana. Sikuwa nimejua naweza kupata watu ambao naweza kujenga urafiki wa karibu jinsi hiyo.
Waadventista huongea kwa upole na upendo, nao wamenifundisha mimi kuishi maisha mema yenye kumtumainia Mungu. Hilo ni muhimu sana kwangu.
Nimekuwepo gerezani kwa miaka mitatu na miezi saba, na miaka miwili ijayo ninaweza kustahili kuwekwa huru niwe uraiani nikitumikia kifungo cha nje. Hilo litawezekana endapo mwenendo wangu utakuwa mzuri. Napenda kudhihirisha kuwa naweza kuaminika na kuwa mtu wa manufaa katika jamii.
Ningeandika ushuhuda binafsi, ningekiri kuwa nimepitia maisha ya huzuni kwa kipindi cha miaka 20. Ni vigumu kwangu kuzungumzia jambo hilo. Familia yangu ilikuwa na matatizo magumu ya kifedha. Hawakuwa karibu nami nilipowahitaji sana kiuchumi. Mambo mengi ya kikatili yamenipata. Hii ndiyo sababu ni mkimya kutokusimulia historia ya maisha yangu.
Iwapo bibi yangu hangalikufa, singaliingia matatizoni hadi kutupwa gerezani. Baada ya kufariki bibi, sikupata malezi sahihi nikawa mkorofi hata kutumbukia kwenye kosa la mauaji.
Baada ya kutoka gerezani, nitapenda kuwa na familia yangu binafsi. Nataka kufanya jambo la manufaa maishani mwangu. Ila kwa sasa mimi ni kijana mkimya nipendaye kusoma shuhuda binafsi.
Asanteni kwa kunisikiliza!!!

Nice one
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom