Mungu inusuru Dar es Salaam Yetu

Amour91

Member
Joined
Mar 9, 2014
Posts
37
Reaction score
23
Ni maumivu na mateso makubwa ndani ya mioyo yetu pale tunapoishi kwa kuogopa au kwa hofu, kwa sasa ndani ya jiji la Dar watu tumekuwa na hofu juu ya ugonjwa wa dengeu kuliko vinginevyo.

Watu wanapata taabu baada ya kuugua ugonjwa huu ambapo baadhi yao pia wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huu, inasikitisha kwani ndani ya jiji letu kuna watu ambao wana maisha ya chini kuliko wengine na kutokumudu kununua neti au kuishi katika mazingira ambayo watakuwa salama juu ya haya.

Lakini ni kwa neema ya Mungu pekee ndiyo yaweza kutuponya na majanga haya. Pole kwa wale waliougua na kuteshwa na gonjwa hili ,Mungu atawakumbuka na pole kwa wale ambao ndugu au jamaa zao wanateseka kwa ugonjwa huu .
 
Amen....mheshimiwa sana alipewaga msaada wa net nje wangegaiwa watu wasio na uwezo wa kununua.
 
Wakati tunamuomba Mungu pia usisahau kufanya hivi
 

Attachments

  • Ngao.jpg
    12.5 KB · Views: 323
Amen....mheshimiwa sana alipewaga msaada wa net nje wangegaiwa watu wasio na uwezo wa kununua.

On top of that kuna zile za hati punguzo sh 500 tu. Sema wengine wanazifanya uzio kwenye bustan zao za mboga.
 
Magonjwa ya milipuko kila leo, kwa kweli hali inatisha sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…