Mungu anapoghairi, anapojuta kwanini alimuumba Mwanadamu na kuamua kumwangamiza...

Guru Master

JF-Expert Member
Jan 14, 2017
224
591
Mungu alipomuumba mwanadamu alikuwa na mpango mzuri.. alimuumba adam na eva akawaweka katika bustani ya eden. ikiwa na hali ya hewa nzuri, ikiwa na wanyama na matunda na kila aina ya uzuri. lengo lake lilikuwa binadamu awe mwangalizi. aishi kwa furaha na upendo akiijaza dunia. alitaka waishi duniani viumbe hawa naye aangalie kazi ya mikono yake. aliwapa utashi. hakutaka wawe kama robots. alitaka wao wenyewe waone umuhimu wake na akaamua katika hilo kuwawekea mbele yao mema na mabaya. na akashauri wachague mema ili wapate kuishi. lakini mwanadamu akamuasi Mungu. toka miaka hiyo tena na tena BINADAMU AMEKUWA NI MUASI.

Tunakuja kuona ndugu wakiuana. Kisa cha Kaini na Habili mauaji ya kwanza kutokea Duniani.
Binadamu aliendelea kuasi

Mungu alitizama chini baada ya miaka kadhaa ya Uumbaji wake wa huyu mwanadamu. Aliona maovu yamezidi. Mungu hakuwaumba wanadamu waishi maisha ya uovu waliyoishi.alitaka waishi kwa upendo, aman na furaha. ni kama Wazaz mnapozaa watoto wenu na kuwalea kwa amani na upendo mkitaka nao waje waishi hivyo lakini mnakuja kuona migogoro,ugomvi na kuuana.wazaz mnaweza juta kwa nini mlizaa watoto .

Mungu Akasikitika na kuwaza "Roho yangu Haitashindana na Mwanadamu Kamwe, Nitamfutilia mbali" na hapo akaamua kuwagharikisha kwa Gharika. Mungu alijiwekea watu kadhaa waje waishi sawa sawa na neno lake. Binadamu aliendelea kumuasi Mungu. Roho ya uasi,usaliti iliwajaa binadamu siku hadi siku. Tukisoma habari za sodoma na gomora na maangamizo mbalimbali kwa njia mbalimbali binadamu aliendelea kukaidi.

Leo hii baba au mama analalamika mtoto wangu kanishida. unadhani Mungu hakuwah kuwaza hilo kwako wewe baba au mama? kwa yale unayomtendea. Mungu anaumia, anaghairi mambo mema kwetu.

1. ADUI mkubwa wa Binadamu SI SIMBA, SI MAMBA. NI BINADAMU MWENYEWE.
angalia vita sehemu mbalimbali duniani.ni binadamu akipigana na binadamu mwenzi. angalia watu wanavyouanana mataifa mbalimbali. wenyewe kwa wenyewe na wenyewe kwa wengine. haya ni mambo ambayo yameshamchosha Mungu. amechoka.

2. UBAKAJI WA WATOTO, WAZEE n.k haya si maisha aliyoyataka Mungu kwa wanadamu. Mungu anajuta kwa nini alimuumba mwanadamu. Mnyama hawezi baka mtoto wake. binadamu anabaka ambaye alipewa akili zaidi ya mnyama.

3. Wanaume na wanawake kuoana. mambo haya yamekuwa ni kichefu chefu mbele za Mungu, yamekuwa mambo ya makwazo. akitizama duniani akayaona haya Mungu anaghairi, Kwanini nilimuumba mwanadamu, kwa nini?" mambo haya yameingizwa hata kwenye baadhi ya nyumba za ibada. huu ni uasi na usaliti mkubwa sana. Mungu amezipima siku za mwanadamu na anaona zimepungua. uovu huu umeingia mpaka ndani ya kanisa. umepewa na kiti cha kifalme ndani ya kanisa. kwa sababu Mungu ni mwenye demokrasia amewaacha watu hawa waishi akiamini kuna siku watabadilika.

4. Tumeshuhudia wamama kuoa watoto wao na wababa nao kuoa mabinti zao. binadamu wamekuwa na akili za kinyama kuliko wanyama. haya hayakuwa makusudi ya Mungu hata kidogo. Mungu aliweka wazi utaratibu ambao alipenda tuishi lakini BINADAMU AMEKUWA MUASI MIAKA NA MIAKA.

5.SILAHA KALI TUNAZOTENGENEZA BINADAMU SI ZA KUULIA WANYAMA WAKALI
. ni silaha za kuulia binadamu wenzetu. angalia vitaa nchi mbalimbali, burundi,kongo,syria,iraq,misri etc. angalia Magaidi wanavyoua watu wasio na hatia kwa kisingizio chochote kile. angalia mataifa makubwa yanavyonyonya madogo. angalia ufisadi unaofanywa na viongoz wetu kwa manufaa yao binafsi. MUNGU AKITIZAMA NA KUONA AMEWAPA NGUVU WAKUBWA WAWASAIDIE WADOGO LAKINI WAKUBWA WANAWAUMIZA WADOGO. anajisikia huzuni, anaumia maana halikuwa lengo lake. Mungu anajuta kwa nini alimuumba mwanadamu.

"mungu alipoona uovu umezidi alisema, roho yangu haitashindana na mwanadamu kamwe, nitamfutilia mbali" hapo akawagharikisha kwa gharika. sodoma na gomora pia walikuwa ni binadamu kama hawa hawa tulio nao. kama mimi na wewe lakini Mungu aliwaondoa kwa moto wa kiberiti. je mimi na wewe tutapateje kupona? tutaponaje? pengine tunaringia elimu, sayansi,utajiri,mamlaka na nguvu zetu. unapokuwa na nyumba unayoipenda sana, ikaanza kuwaka moto ndugu yangu utafanyaje? kimbia hatari.
 
sio kweli mkuu, kama yeye ni muumbaji wa kila kitu na anajua yote yajayo (kwa mujibu wa vitabu)sasa kulikuwa na umuhimu gani wa kuumba wakati haya yote aliyajua kabla?na kama ni muweza wa yote kwanini asizuie kabla na uwezo wa kuzuia alikuwa nao?take it from me Mungu yupo ila siyo huyo wa kwenye bible na quran ambaye anaumba viumbe yeye mwenyewe kisha anakasirika kwa kazi aliyoifanya mwenyewe?
 
Hivi Ina Maana Huyu Mungu hakujua kama Haya yatatokea?
 
sio kweli mkuu, kama yeye ni muumbaji wa kila kitu na anajua yote yajayo (kwa mujibu wa vitabu)sasa kulikuwa na umuhimu gani wa kuumba wakati haya yote aliyajua kabla?na kama ni muweza wa yote kwanini asizuie kabla na uwezo wa kuzuia alikuwa nao?take it from me Mungu yupo ila siyo huyo wa kwenye bible na quran ambaye anaumba viumbe yeye mwenyewe kisha anakasirika kwa kazi aliyoifanya mwenyewe?
Huyo Mungu mwengine habari zake zinapatikana wapi?
 
It is easy to fool people than to convince them that they've been fooled.

GOD DOES NOT EXIST!!!!!
Unajua ukiacha Mungu anayelezwa kwenye Biblia na Qur'an bado pia kuna miungu mengine ambayo ni tofauti na aliyeelezwa kwenye Qur'an na Biblia...sasa wewe unaposema tu Mungu haja exist unamkusudia mungu gani?
 
Hii dunia ilikuwa na mamilioni ya miungu kama vile Odin, Thor, Ra,Frey, Baal n.k.

Hiyo miungu haina tatizo maana zipo shahidi za kuwepo kwao. Lakini huyu Mungu wenu wa kwenye vitabu aliyesafirishwa kwa mashua hadi Africa ndiyo mwenye utata wa uwepo wake.

Linapoibuka swala la Mungu huwa tunam-refer huyo Mungu mnayedhania yupo maana waamini wake wanadai kuwa yeye ndiyo Mungu na hakuna kama yeye.
 
Sasa we unahisi hayupo au una uhakika kuwa hayupo?
 
Tofauti ya kuhisi kutokuwepo kwa Mungu na kuwa na hakika ya kutokuwepo kwa Mungu ni nini?
Labda kuna mambo ambayo wewe binafsi unaoona hayako sawa kuhusu mungu anayeelezwa kwenye vitabu na hali hiyo ikakufanya uhisi kuwa huyo mungu hayupo lakini ndiyo huna uhakika,na kuwa na uhakika ni kuwa na ushahidi ya kuwa mungu hayupo.
 
Mungu anajua mwanzo mpaka mwisho sasa kwa nini alimuumba shetani huku akijua kwamba atakuja kuharibu? Kwa nini aliweka mti wa kati eden huku akijua kwamba Adam na Eva watakula tu? Kwa nini alimtupa shetani duniani na si sayari nyingine ambazo hazina viumbe au galaxy nyingine ili kutuokoa wanadamu?

Kwa nini hakumuangamiza shetani baada tu ya kuasi kwa sababu kama aliweza kuwashawishi malaika kuasi basi binadamu hatukua na nafasi ya kushinda vishawishi. Kwa nini makosa ya Adam yanihusu mimi wakati sikula tunda? Kila mtu atabeba mzigo wake mwenyewe. Kwa nini hakudeal na Adam na Eva baada ya uasi akaacha wakazaliana huku wengine tukiishia kuwa tu victims au collateral wakati real culprit ni shetani, Adam, Eva.
 
Labda kuna mambo ambayo wewe binafsi unaoona hayako sawa kuhusu mungu anayeelezwa kwenye vitabu na hali hiyo ikakufanya uhisi kuwa huyo mungu hayupo lakini ndiyo huna uhakika,na kuwa na uhakika ni kuwa na ushahidi ya kuwa mungu hayupo.
Kazi ya ku-prove uwepo wa Mungu ni ya watu wanaoamini uwepo wa Mungu.

Huwezi kumwambia mtu asiyeamini uwepo wa Mungu atoe ushahidi wa kutokuwepo kwa Mungu, ingawa anaweza kutoa sababu za kutokukubaliana na idea ya uwepo wa Mungu. Sababu hizo zilishatolewa hapa JF na wajumbe mbalimbali lakini hakuna ushahidi uliojitosheleza kimatiki, kiuhalisia na kisayansi wa kuwepo kwa Mungu niliowahi kuona popote.
 
Ndiyo maana nikasema unahisi kuwa hakuna mungu na si kwamba una uhakika kuwa hakuna mungu. Maana hata wanaosema mungu yupo wanaamini,sasa wewe ukisema una hakika halafu uhakika wenyewe unategemea wenyekuamini uwepo wa mungu hapo itakuwa umelitumia vibaya neno hakika.
 
Swala siyo uhakika ama hisia bali kinachotakiwa ni ushahidi wa uwepo wa Mungu. Tofauti na hapo hakuna kitu.
 
Hoja yangu ni hilo dai lako kwamba una uhakika mungu hayupo,umeshindwa kutuoa huo uhakika uliyonao ambao unakufanya useme hakuna mungu. Watu washatoa sababu kibao tu za kwanini wanaamini mungu ila wewe unasema una hakika hayupo.
 
Back
Top Bottom