Mungu amsikilize nani?

ZENITH

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2012
Posts
1,064
Reaction score
991

Ungekuwa wewe ndo mungu ungejibu sara ya yupi?mpiga penati au golikipa?
 
siku zote nasema kuiombea timu ishinde ni upuuzi
 
ambae ameelemewa ningemsikia.lakini bahati mbaya siwezi kuwa mungu labda ningekuwa refa hapo kingeeleweka.
 
Kwa vile wote ni viumbe wake basi awasikilize wote kwa vile haishiwi neema. Simpo akiwasiliza wanatoka draw and that is that.
 
Hapo ndipo mungu atakapohitaji Quantum Physics.

Katika Quantum Physics inawezekana goli likafungwa kwa penati na kipa akazuia penati hiyohiyo vilevile.

Lakini bottom line mungu ambaye hayupo hawezi kumsikiliza mtu.
 
Ndo maana MUNGU amejificha,longolongo hizi wabongo si mngekuwa mnaandamana daily kwenda kwake!?
 
Ambaye ni msafi kati yao maana Mungu hasikilizi maombi ya mwenye dhambi kwa mujibu wa Biblia.
 
ambae ameelemewa ningemsikia.lakini bahati mbaya siwezi kuwa mungu labda ningekuwa refa hapo kingeeleweka.
mmmh!!hii picha ishakuwa avatar!!! taamu salama??
 
Last edited by a moderator:
Mungu yupo busy haangaiki na mambo madogo madogo kama hayo.

Sent from my GT-S5570 using Tapatalk 2
 
Atawaadhibu wote wawili vikali. Unajua kucheza mpira ni dhambi?

Wengi yawezekana hamjui, lakini acha niwakumbushe kuwa kumpiga mwenzio chenga lazima umdanganye kwamba unaenda huku, lkn badala yake unaenda the other side. UONGO unavunja amri ya ngapi, kila mtu anajua
 
hapo unakuta wameshakatiza kwa Mtaalamu
 
Double Standard, Mungu humpa aombaye kwa Imani
 
''lakini si kama tutakavyo sisi,bali mapenzi yake yatimizwe''
 
Mungu atakaa pembeni ataacha bahati ichukue nafasi.
 
Ambaye ni msafi kati yao maana Mungu hasikilizi maombi ya mwenye dhambi kwa mujibu wa Biblia.

Kweli Mungu hasikilizi wenye dhambi? Naomba hiyo verse kwenye biblia nijiridhishe mkuu
 
Kweli Mungu hasikilizi wenye dhambi? Naomba hiyo verse kwenye biblia nijiridhishe mkuu

Nikikumbuka au nikiupata nitakuwekea ipo mistari mingi inayosema hivyo. Ila kama sijakosea ukisoma kwenye Isaya, Yeremia na Zaburi unaweza ukaipata. Unaweza kusoma pia Zaburi ya 34 kama inaweza kuwepo sina Biblia karibu yangu kwa ajili ya kufanya rejea ya uhakika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…