pipinpadiloxicopolis
Member
- Aug 25, 2013
- 27
- 6
Basi lenye watu ishirini wenye sura mbaya lilipata ajali na abiria wake wote kufariki dunia.Walipofika mbinguni Mungu akawaambia"kwakua mliishi maisha ya kuchekwa kutokana na sura zenu,nitampa kila mmoja wenu nafasi moja ya kuniomba atakacho nami nitamtimizia".Wakwanza akaomba awe handsome,wapili akaomba awe mwanamke mzuri sana,waliofuata nao wakiomba kati ya vitu hivyo viwili.Lakini kuna mmoja wao alikua amesimama pembeni akicheka,Mungu akamuuliza "unacheka nn?",nae hakujibu chochote.Alibakia yy wa mwisho na alipoenda kuomba atakacho,Mungu akamwambia "nawe sema utakacho nikamilishe furaha yako". Jamaa akamwambia Mungu "naomba uwarudishie walionitangulia sura zao".
Je ww ungekua miongoni mwa wale 19 ungefanya nn?
Je ww ungekua miongoni mwa wale 19 ungefanya nn?