Mume wangu anachepuka

Pole dada yangu kwa unayo pitia.
Binafsi sipendi kuwa wa kwanza kumuambia mtu atoke kwake ila:
Kama hujafunga ndoa na huna mtoto; Hapo mungu anakuonesha kuwa huyo sio muoaji/mume
Naomba ukimbie haraka...
Kama hujitegemei...jitahidi akupatie mtaji/kianzio halafu uchape lapa
 
hujaulewa bado unaumiza kichwa na kujizeesha bure kwa majukumu ya wife kabla hujawa wife n una umri mdooogo sana unavumilia amekuwa baba yako huyo??????????????
 

Ninyi bado ni watoto
Endeleeni kucheza
Ndoa si masihara......
 

Dawa ya moto ni moto
 
Eeh pole sana, Sina cha kushauri make cha kufanya unakijua wewe....
 
Hujaolewa stress ndo hizo.

Sepa bwana.
 
Ahaaaaa ur too young 4 those sheet mdg wangu na kimbia hatari huna mtt anakuchosha ukiwa nao wanne si atakumbia? Ifike mahali wanawake muone taa nyekundu my take ur time ur too young 4 that sheet unaogopa kuanza maisha ur too young!!
 
Naomba ujipende, wafikirie wazazi wako waliokuzaa walivyokuthamini na wanavyokupenda. Huyo ni nani tena hajakuoa bado anakufanyia ushenzi ushenzi, una kilema gani wewe kwamba hutapata wa kukupenda. Usimwache akupotezee muda wa ujana wako. Ondoka kabla hajakusababishia maradhi yasiyopona ukajuta zaidi ya muda uliopoteza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…