JustDoItNow
JF-Expert Member
- Dec 3, 2013
- 2,967
- 1,513
Inasemekana Rwanda ni kama Isreal ya Afrika...Mimi sina shida kama anafanya haya kwa ajiri ya Waafrika wote wa Rwanda, lakini kama anafanya haya kwa ajiri ya ubinafsi hapo apigwe vita.
Israel na rwanda ni vitu viwili tofauti kabisa.
1. Israel kuna koo(makabila) zaidi ya kumi ambayo yanachangamana kwa kila jambo, rwanda makabila makuu mawili ambao wanaishi kama paka na panya. Hawapendani kabisa.
2. WaIsraeli wana dini yao tofauti na ukristu na uislam. Rwanda wamo kwenye dini za kikristu na kiislam etc. Hawana Dini yao special
3. Waisrael wametapakaa dunia nzima na kuunda umoja wao kwa msingi ya uisrael. Rwanda hata kama wametapakaa hawana umoja ugenini kwa misingi ya nchi ya rwanda, ni kwa misingi ya uhutu na utusi.
4. Matajiri wakubwa kwenye nchi zilizosimama kiuchumi kama USA, RUSSIA na nchi nyingi za ulaya wengi wana asili ya kiyahudi. Rwanda haijafikia kiwango hicho.
Ndo maana unaona Israel ni ka nchi kadogo lakini kana nguvu sana. Haya mambo hayaji ki juu juu tu mkuu. N imeichukua muda mrefu sana.