Mume ,mke waua mtoto wakipigana

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,864
155,818
KAMPALA,Uganda

JESHI la Polisi nchini Uganda linawashikilia mtu na mkewe kwa tuhuma za muaji ya mtoto wao mwenye umri wa mwaka mmoja wakati wakigombana katika ugomvi wa ndani ya familia.

Jeshi hilo la Polisi limesema kuwa,mtoto huyo aliuuawa baada ya Anifa Namayanja, (27),kumtumia kama ngao wakati akipigana na mumewe,Sam Buyinza, 36.

Msemaji wa Polisi wa Jiji la Kampala,Henry Kalulu,aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa wiki iliyopita Buyinza alimuua mwanaye huyo, Kisaakye Byakatonda wakati akigombana na mkewe ndani ya nyumbani yao iliyopo eneo la eneo la Kisigula lililopo kata ya Mutundwe,nje kidogo ya jiji la Kampala.

Msemaji wa huyo wa Polisi alisema kuwa baada ya kubaini kuwa mwanaye amejeruhiwa, Buyinza alimkimbiza kwenye Zahanati na alichoambuliwa ni kuelezwa kuwa mtoto huyo alikuwa amekwishafariki.

Alisema, wakati Buyiza akimkimbiza hospitalini mtoto huyo, Namayanja wakati huo alikuwa amekwishakimbia nyumbani na kamanda Kalulu alisema kuwa wanandoa hao watafunguliwa mashtaka ya mauaji.

Akielezea tukio hilo zaidi, Kamanda Kalulu alisema kuwa baada ya kutokea hali hiyo Buyinza ambaye ni muendesha pikipiki za kukodi maarufu kama boda-boda alitoa taarifa katika kituo cha Polisi cha Nalumunye ambako alitiwa mbaroni na baadaye Polisi wakafanikiwa kumnasa Namayanja na kisha wanandoa hao kusafirishwa hadi Kituo cha Polisi cha Kajjansi.

Msemaji huyo wa Polisi alisema kuwa mwili wa mtoto huyo umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika hospitali ya Mulago kwa ajili ya kufanyiwa uchunguzi.

Akielezea kuhusu tukio hilo, Buyinza aliomba msamaha huku akieleza kuwa bado anahitaji kuzaa tena na akasema kuwa ugomvi huo ulisababishwa na ulevi.


“Nimewahi kurejea nyumbani mara kadhaa na watoto wakanieleza kuwa mama yao ameenda kunywa pombe na kabla ya siku ya tukio alirejea nyumbani akiwa amelewa na siku iliyofuata ikawa hivyo hivyo na siku ya tukio aliamua kutoweka tena wakati nilipokwenda kazini hivyo na mimi nikaamua kuondoka nikaenda kunywa waragi,”alisema Buyinza.

Alisema kuwa alinunua pakti tatu za pombe aina Vodka kutoka duka jirani kabla ya ugomvi huo kufumuka na kasema kuwa wala hakudhamiria kumpiga mwanaye.

“Samahani kwa yote yaliyotokea ila nahitaji kusamehewa na kuacha pombe kwa sababu ndizo zilizonisababishia kufanya hivi,” alieleza Buyinza.

Kwa upande wake Namayanja alikiri kunywa pombe mara kadhaa lakini akasema kuwa alikuwa hajanywa pombe siku ambayo Buyinza alimtembezea kisago.

Aliwaonesha waandishi wa habari mikwaruzo shingoni na mikononi akisema kuwa mumewe alikuwa akijaribu kumvunja na kumkaba shingo huku akikana kumuua mwanaye.


http://darleo.co.tz/index.php?option=com_banners&task=click&bid=9
 
Back
Top Bottom