Naombeni ushauri,
Mimi mume wangu simuelewi kabisa. Historia kwa ufupi iko hivi nilianza kuishi na mume wangu mwaka 2010, kitendo cha kubeba ujauzito mwanangu wa 1 alifurahi sana. Kipindi cha kunyonyesha nyumba iliwaka moto mwanaume mkali analala nje haitoshi anatembea hadi na mpangaji mwenzetu yote niliyavumilia.
Kufika mwaka 2013 ugomvi ukaanza tena pombe wanawake ndo ugonjwa wake kuna mwanamke nilimjua anatoka nae nikagombana naye sana. Baada ya mume wangu kujua akasema tuachane. Nikamuomba yaishe tusiachane akagoma. Hasikii cha wazazi wala marafiki wa familia.
Basi akanifukuza eti mtoto atamlea tu kwa kutuma pesa. Bahati nzuri nina rafiki yangu yeye ni msomi kidogo akaniambia nikamfungulie kesi ya fidia kwa miaka yote niliyoishi naye.
Kumbuka hapo tuna gari na nyumba inajengwa bado haijakamilika. Basi kesi ilfika hadi mahakamani huyu mume kuulizwa kama yuko tayari kuachana akasema ndio yuko sikuamini kabisa hadi nikajiuliza kwanini mimi.
Na yeye kosa kubwa analodai kwamba mimi ni mkorofi wivu umezidi namtia aibu kwa rafiki zake kwa kuwahisi ni hawara zake. Basi mahakama ikaniuliza mimi kama nina chochote cha kusema. Nikawambia basi kama hanitaki tena ninacho omba stahiki zangu nilimkuta hana gari wala nyumba na viwanja 2 tumenunua tukiwa wote.
Mahakama ikaamuru kila kitu tugawane asilimia 50 kwa 50 kwa kuwa tumeishi zaidi ya miaka 2 hivyo hiyo ni ndoa halali na kuhusu mtoto atakuwa akikatwa pesa kazin Tsh 5000 kwa siku kwa ajili ya mtoto hivyo barua niipeleke ustawi. Mume wangu kusikia hivyo akasema anataka rufaa basi wakamruhusu.
Cha ajabu rufaa asikate akaanza kuomba msamaha anawapigia simu wazazi wake wamuombee msamaha kawa mpolee. Kiukweli nilimsamehe tukaishi kama zamani akanifungulia duka la biashara tukahamia kwenye nyumba yetu tukabariki ndoa kanisani. Cha ajabu toka mwaka huu uanze tabia zimerudi upya kulewa anarudi saa 8 au 9 usiku.
Kuna siku nilimuomba simi yake niongee na mama huwezi amini macho hayana pazia gallery nikakuta picha za msichana yuko uchi. Nikapekua zaidi whatsapp uyo binti ni mke wa mtu kaja Dar es Salaam kutoka Mbeya kimasomo mumewe yuko Zanzibar.
Hivi ninavyowambia tumetengana vyumba na anaforce nizae mtoto wa 2 hata muda mwingine ananilazimisha tendo la ndoa. Ndugu zangu naombeni ushauri. Mimi binafsi natamani nikaanze upya maisha yangu.