Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es salaam Jumanne Muliro amejibu madai ya wanaharakati wawili kutoka Uganda, Agather Atuhaire (Uganda na Boniface Mwangi (Kenya) kuwa waliteswa walipokuwa Tanzania, akisema hayo ni maoni yao na kama wana malalamiko waende kushitaki kwenye mamlaka husika.
Ameyasema hayo alipohojiwa na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC).
Mwangi na Atuhaire walikuwa miongoni mwa wanaharakati waliokwenda Dar es Salaam kuhudhuria kutajwa kwa kesi ya uhaini inayomkabili mwenyekiti wa chama cha upinzani nchini Tanzania CHADEMA Tundu Lissu.
Ukisikiliza ni kama anajikanyaga sana kujibu, halafu cha kuchekesha anasema eti hayo ni maoni yao, hivi Agatha na Boniphace walikuwa wanatoa maoni gani kwenye ile press?
Wale walikuwa wakitoa taarifa ya nini kiliwasibu baada ya kukamatwa... hivi huyo mzee anaelewa hata maana ya maoni kweli?
Sidhani kama wanatoa maoni hao jamaa wa Kenya na Uganda, wanatoa taarifa ya kile kilichowakuta Tanzania walipokamatwa na vyombo vya dola.
Hata kama yangekua maoni, kwani Muliro alitaka watoe maoni ya jeshi la polisi au ya kwake yaye Muliro? Si bado yangekua maoni yao hao kina Boniface? Muliro vp kamanda, umechanganyikiwa nn!