Rutunga M
JF-Expert Member
- Mar 16, 2009
- 1,769
- 1,390
Diwani wa kata ya ikondo wilayani Muleba Mkoani Kagera Bw Felician Rutwaza(pichani) amejiuzulu nafasi ya ujumbe wa kamati ya uchumi na fedha ya Baraza la Madiwani wa Halmashauri hiyo baada ya kamati hiyo kujiingiza katika masuala ya rushwa na kutumia kamati hiyo katika masuala binafsi badala ya kuendeleza Halmashauri hiyo.
Tayari Diwani huyo amekwisha andika barua rasmi ya kujiuzulu kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Muleba Bw Kamugisha amedhibitisha kupokea barua ya diwani huyo kujiuzulu lakini akasema yuko nje ya ofisi na kwamba atakuwa na la kusema baada ya kufika ofisini.
"Niko nje ya ofisi na nimesikia hiyo barua iko ofisini kwangu,nikifika nitakuwa na la kusema lakini kwa sasa siwezi liongelea kwa undani" Alisema diwani huyo wakati akihojiwa na Mtandao huu kwa Simu.
Hata hivyo Diwani Rutwaza akiongea na mwandishi wa habari wa mtandao huu amesema ni kweli amejiuzulu lakini hawezi kuongea kwa undani sababu zilizosababisha ajiuzulu.
"Ni kweli nimejiuzulu nafasi hiyo na mamlaka husika nimekwisha kabidhi barua,unaweza kuwauliza kwa ufafanuzi lakini mimi siwezi sema zaidi"Alisema Lutwaza wakati akihojiwa na Mtandao huu.
Chanzo: Breaking News