Mukama aiaibisha serikali ya chama chake: hamtambui Ghadafi

zimmerman

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
1,448
2,640
Kama tunavyofahamu serikali ya Tanzania kupitia Waziri wake wa Mambo ya Nje, Bernard Membe haiutambui utawala wa sasa unaotawala Libya Nationa Transitional Council (NTC) kwa hivyo bado inautambua utawala uliopita wa bwana Muammar Ghadafi. La kushangaza Katibu Mkuu wa chama kinachoshika hatamu ya serikali ya Tanzania, CCM, jana amepingana na serikali yake waziwazi kwa kauli yake dhidi ya Chadema, huku akikifananisha Chadema na utawala dhalimu wa kifamilia wa Ghadafi. Kwa maneno yake Mukama nikinukuu gazeti la Mwananchi leo "Uongozi wa Chadema unatofautianaje na wa Gaddafi (Muammar)?"

Maoni yangu:

Mukama na serikali ya chama chake wanadhihirisha ile kauli ya Baba wa Taifa kwamba "Chama dhaifu huzaa serikali dhaifu". Hapa tunamwona Mzee Mukama akisema maneno ambayo waziwazi yanamwonyesha kama mtu ambaye anakurupuka kusema kila kinachomjia kichwani kwa wakati huo bila kujali kinaiweka serikali yake katika nafasi gani hasa ukizingatia sera zake kwa mambo ya ndani au nje ya nchi.

Ni jana yake tena amesema maneno ya kuliaibisha jeshi la polisi kwa kuituhumu Chadema kuingiza makomandoo waliofunzwa ugaidi huko Afghanistan, Palestina na Libya. Hata hivyo jeshi la Polisi lilikwepa aibu hiyo kwa kukanusha madai ya Mukama.

Wana Igunga kuna ushahidi gani mwingine zaidi wa kukikataa Chama Cha Mapinduzi kwa kauli hizi za viongozi wake wakuu wasioweza kufikiria waseme nini kwa watu gani na kwa wakati gani?

Kama CCM wanasema uongo sasa wakati wa kampeni; nina uhakika gani huyo mgombea wao wa ubunge anawaahidi ya ukweli atakayokuja kuyatekeleza?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom