PreGE2025 Muinja Maingu: Vijana tusiwaachie Wazee Siasa, tupambane!

PreGE2025 Muinja Maingu: Vijana tusiwaachie Wazee Siasa, tupambane!

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

upupu255

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
341
Reaction score
476
Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) katika Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka, na mdau wa maendeleo Musoma Vijijini, Muinja Maingu, amesema pamoja na vijana kuwa kundi kubwa katika jamii, bado wamekuwa na ushiriki mdogo katika siasa na kuwaachia wazee, jambo ambalo linaweza kuwa na athari kwa kesho ya taifa.

1742211372536.png
Maingu ameeleza kuwa ni lazima vijana washiriki katika maamuzi ya kisiasa na kuacha dhana ya kuamini kuwa siasa ni kwa ajili ya wazee pekee, ili kuleta mabadiliko chanya yanayoendana na teknolojia ya sasa katika jamii zao.

Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Amewataka vijana kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi pamoja na kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura ili wawe na sifa ya kuchagua au kuchaguliwa katika uchaguzi ujao.
 
Back
Top Bottom