Muhsin Abdallah (Sheni) Ameinunua Nchi Hii?

Wambugani

JF-Expert Member
Dec 8, 2007
1,757
276
Ni ukodishaji vitalu kinyemela
Unahusu Shilingi. bilioni 11
Msemaji Mkuu wa kambi ya Upinzani wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee

Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni imefichua ufisadi mkubwa wa mamilioni ya dola za Marekani zinazodaiwa kutaka kuibwa kupitia mkataba wa siri uliofikiwa baina ya kampuni moja ya uwindaji ya Kitanzania na kampuni mbili za kigeni kwa ajili ya kufanya utafiti wa uchimbaji wa madini ya urani kinyume cha sheria ya matumizi ya ardhi.

Kampuni hiyo ya uwindaji imetajwa kwa jina la Game Frontiers of Tanzania Limited inayomilikiwa na Mohsin M. Abdallah na Nargis M. Abdallah.

Kampuni hiyo inadaiwa kuingia mkataba na kampuni za Uranium Resources PLC na Western Metals Limited, kwa ajili ya kazi hiyo, katika kijiji cha Mbarang’andu, kilichoko katika wilaya ya Namtumbo, mkoani Ruvuma.

Ufisadi huo uliibuliwa na Msemaji Mkuu wa kambi hiyo wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Halima Mdee, wakati akiwasilisha hotuba yake kuhusu mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2011/2012 na makadirio ya matumizi ya wizara hiyo kwa mwaka 2012/13, bungeni jana iliyokuwa imewasilishwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka.

Kwa mujibu wa Mdee, mkataba huo ulitengenezwa na kampuni ya wanasheria ya Kitanzania ya Rex Attorneys na kwamba, ulisainiwa Machi 23, 2007, huku vipengele vyake vikiainisha kwamba, unatakiwa uwe wa siri.

Mdee alisema kwa mujibu wa mkataba huo, malipo yaliyoafikiwa baina ya kampuni hizo kwa kazi hiyo ni ya dola za Marekani milioni sita (sawa na Sh. bilioni 9.6), ambazo zitalipwa kwa awamu mbili.

Kwa mujibu wa Mdee, malipo ya kwanza, yatafanyika pale uzalishaji wa urani utakapoanza.

Alisema malipo mengine ni ya dola za Marekani 250,000 (Sh. milioni 400), ambayo kampuni hizo zimekubaliana ni ya baada ya kampuni za madini kukamilisha utafiti wa urani na kupata kibali cha uchimbaji.

Malipo mengine alisema ni ya dola za Marekani 55,000 (Sh. milioni 88) kila mwaka kama fidia ya kushindwa kufanya biashara na usumbufu unaotokana na shughuli za machimbo kwenye kitalu na kwamba malipo hayo yatafanyika kila Machi 31.

Mengine ni ya dola za Marekani 10,000 (Sh. milioni 16) kwa vijiji vitakavyoathiriwa na utafiti wa urani.

Hata hivyo, Mdee, alisema wakati kampuni hiyo ya uwindaji ikiingia mkataba huo wa siri, sheria ya zamani ya uhifadhi wa wanyamapori ya mwaka 1974 na sheria mpya namba 5 ya mwaka 2009 zinamruhusu mtu aliye na leseni ya uwindaji kuwinda wanyama tu na siyo vinginevyo.

Alisema pia sheria namba 4 ya ardhi ya mwaka 1999 na sheria namba 5 ya ardhi ya vijiji ya mwaka huo, zinatamka bayana kwamba ardhi inajumuisha vitu vyote vilivyo juu ya ardhi na chini ya ardhi isipokuwa madini au mafuta.

“Na kwa mujibu wa sheria za Tanzania linapokuja suala la madini, umiliki unatoka kwa mtu binafsi na kurudi serikalini. “Na ni serikali kupitia Wizara ya Nishati na Madini ndiyo pekee yenye mamlaka ya kutoa leseni ya kutafuta madini kwa kampuni za madini,” alisema Mdee.

Kutokana na hali hiyo, aliitaka serikali kueleza uhalali wa mkataba baina kampuni hizo na kueleza sheria inayoipa kampuni ya uwindaji haki ya kualika kampuni ya nje kwenye eneo ambalo haina umiliki kufanya utafiti na hatimaye kuchimba madini hatari ya urani.

Pia aliitaka serikali kueleza nini mustakabali wa Watanzania wanaoishi kwenye vijiji vinavyozunguka mbuga hiyo, ambao wanaishi maisha yao ya kila siku pasipo kujua kama kuna utafiti wa madini hatari ya urani unaoendeshwa kwa siri kubwa.

“Ni serikali gani yenye uwakilishi mpaka ngazi ya kitongoji na usalama wa taifa mpaka ngazi ya chini kabisa za utawala inashindwa kuyaona haya?” alihoji Mdee.

Pia aliitaka serikali kuangalia hatua za kuchukua dhidi ya wawekezaji katika mashamba 13 walioshindwa kuyaendeleza kwa asilimia 100, pamoja na wawekezaji katika mashamba 14 walioshindwa kabisa kuendeleza mashamba waliyonunua.

Alitoa mfano kwa mwekezaji anayejiita Chavda Group aliuziwa mashamba saba yenye ukubwa wa hekta 25,000 kwa bei ya kutupa katika maeneo tofauti nchini, ambapo kikubwa alichokifanya ni kutumia hati za shamba kuchukulia mikopo kisha kuyatekeleza.

“Hivi kweli unahitaji kuwa na akili nyingi kuyaona haya? Nyuma ya Chavda Group wako kina nani?” alihoji Mdee na kuongeza:

“Ni familia hii hii ya Chavda (V.G. Chavda na kaka yake P.G. Chavda) waliojitwalia mkopo wa dola za Marekani milioni 3.5 mwaka 1993 chini ya DCP (Dept Conversion Program) wakiahidi kufufua mashamba ya mkonge Tanga ndani ya miaka 10 na kupata dola za Marekani milioni 42.

“Walipopata mapesa hawakufanya lolote na hakuna hatua zozote zilizochukuliwa dhidi yao. Kwa utaratibu huu, lazima tuwachukulie wawekezaji wa aina hii kama ni ‘waporaji’ na hawana tofauti na majambazi yanayoiba benki kwa kutumia nguvu.”

Aliitaka serikali kupitia wizara hiyo kusimamia sekta ya ardhi kuhakikisha kwamba maeneo yote ambayo hayajaendelezwa na wawekezaji yanarejeshwa serikalini bure bila fidia kwa ajili ya kutafuta wawekezaji wengine wenye mtaji wa kutosha watakaoyaendeleza mashamba hayo.

Alisema kwa mashamba ambayo tayari yana wakulima wadogo wadogo wanaoendesha shughuli zao za kilimo, serikali ipange utaratibu wa kuwamilikisha maeneo husika ili kuondokana na dhana ya ‘uvamizi’ au kukodishwa ardhi kwa ajili ya kilimo.

Mdee alisema zoezi hilo lazima lifanywe kwa uwazi ili kuepuka udanganyifu uliotokea katika maeneo mengine nchini, ambapo vigogo na watu wenye nafasi zao walijitwalia ardhi wakijifanya na wao ni sehemu ya wanakijiji.

Source: NIPASHE
 
Wafugaji wa Kijiji cha Vilima Vitatu, Wilayani Babati wanaishi kama squatters kutokana na Kitalu la Bwana Sheni
na yeye huwinda mpaka kwenye sehemu wanazoishi wenyeji.
 
huwa sielewi hawa watu wanaibomoa hii nchi kwa faida ya nani?!!!sijui kama akili zao ziko sawa
 
this country!
huwa sielewi hawa watu wanaibomoa hii nchi kwa faida ya nani?!!!sijui kama akili zao ziko sawa
Mh. Halima Mdee anaweza kuonewa huruma na wengi wetu kuwa 'mdomo wake utamponza', hizi ndizo slogans za Watanzania tulio wengi ambao hupenda kuvuna bila kulima, kupanda na kupalilia. Na hao ndio hawaelewi ni kwa nini Dr. Stephen Ulimboka yuko hospitalini hivi sasa.
Nchi hii inataka majasiri na sio utani.
 
Wafugaji wa Kijiji cha Vilima Vitatu, Wilayani Babati wanaishi kama squatters kutokana na Kitalu la Bwana Sheni
na yeye huwinda mpaka kwenye sehemu wanazoishi wenyeji.

Tukiwaambia kuwa ccm ni chama cha mafisadi mnabisha; ona sasa mambo anayofanya huyu Sheni kuihujumu hii nchi ili hali na yeye ni mjumbe wa NEC ya ccm!!! Nchi hii itapona kweli kwa mtindo huu?
 
Sasa nimefahamu kwanini watu hujifunga hydrogen peroxide na...... ooops! Mbona nataka kutoboa siri zangu kwa Jack Zoka....subirini muone, tutajilipua katikati ya vikao na mikutano yenu! Hizo electric fences zenu haziwezi kutuzuia! Tumechoka na ufisadi!
 
Cha mjinga huliwa na mwerevu yes lakin ....

Mjinga akielevuka, mwerevu yupo mashani.

CCM ijitafakali na ijipime kwasababu hata paka/nyau ukimbana kisawasawa kwenye kona ya nyumba hugeuka kuwa hatari isiyo na kipimo japo mdogo na mnyonge aweza kuuwa kwa kukung'ata koo baada ya kukurukia akijihami.

Vijana wa kizazi hiki wamepigika kimaisha na kama paka aliebanwa, sitoshangaa aslan siku moja kushuhudia mauwaji ya wanasiasa hapa tz kwa kujitoa mhanga.

Zama za kidum chama na fikra za mwenyekiti wa ccm hata kama za kipuuzi zimepita na hazina nafasi kwa jamii ya sasa.

Ulafi na ubinafsi wa watawala upo ukingon na kwa bahati mbaya hatari inayowakabili wanaipuuza kwa mtazamo wa paka hawezi kumuadhiri mwenye nyumba.
 
wa kutoka south afrika wamenunua, Bush & co. wamenunua, akina Clinton, Bill gates, waingereza, wayahudi pia, hahaha, Leo imekuwa ajabu mtanzania kununua?. Au Sababu anaitwa Muhsin Abdallah?. Wawekezaji waliokuja kuchimba mawe hamuwataji namna walivo nunua ardhi ya Tanzania. Jameni uadilifu kitu muhimu. Musifanye jambo ikaonekana munaelemea upande mmoja. Review ya wawekezaji inahitajika kusudi ya kupinga kudhalilishwa kwa wananchi walalahoi. Mtindo wa kuuzauza lazima usimamishwe maana imekuwa ni matatizo makubwa na hasa kwa kizazi kijacho.
 
wa kutoka south afrika wamenunua, Bush & co. wamenunua, akina Clinton, Bill gates, waingereza, wayahudi pia, hahaha, Leo imekuwa ajabu mtanzania kununua?. Au Sababu anaitwa Muhsin Abdallah?. Wawekezaji waliokuja kuchimba mawe hamuwataji namna walivo nunua ardhi ya Tanzania. Jameni uadilifu kitu muhimu. Musifanye jambo ikaonekana munaelemea upande mmoja. Review ya wawekezaji inahitajika kusudi ya kupinga kudhalilishwa kwa wananchi walalahoi. Mtindo wa kuuzauza lazima usimamishwe maana imekuwa ni matatizo makubwa na hasa kwa kizazi kijacho.


Mkuu, tunajadili
Uhalali kama taratibu zimefuatwa kwa maslahi ya watanzania.

Kama clinton, wayahud, wasouth nk wameuziwa na taratibu hazikufuatwa nimakosa pia, lakin kama zilifuatwa ni jambo lingine.

Tunajadili mikataba feki ya siri na kifisadi. Mikataba inayolenga kutunyima haki yetu ya msingi kikatiba kugawana laslimali zetu kwa uwazi na kutunufaisha sote, sio shein peke yake au hao uliowataja.

Wengi wetu tunaumwa na ufisad ww je?
 
Back
Top Bottom