Gold Member JF
Member
- Nov 14, 2013
- 5
- 0
SERIKALI imesema hadi kufikia Oktoba mwaka 2014 karibu vituo vyote vya kuzalisha umeme jijini Dar es Salaam vitakuwa vimekamilika. Vituo hivyo ni pamoja na Kinyerezi One, Kipawa, Gongolamboto na Mbagala. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kukamilika kwa mradi huo kutawezesha kuzalisha megawatt 1,500 na kufikia megawatt 3,000 pamoja na zile za awali.
Itakuwa ni faraja kubwa kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam, hususan wananchi waishio maeneo ya Kinyerezi, Mbagala, Kipawa, Gongolamboto na katika ya jiji kwani watakuwa na uhakika wa kupata nishati ya umeme kila siku bila matatizo yoyote.
Mitambo hii itaongozwa na mashine za kisasa za kurekebisha tatizo lolote endapo kutatokea hitilafu ya umeme, pia kuna mbadala wa mafuta endapo gesi itakuwa na shaka,alisema.
Alisema licha ya serikali kuchangia katika miradi miwili tu kati ya minne, bado kuna umuhimu wa kuendelea kuweka ubia katika miradi hiyo .
Ingawa ni miradi miwili pekee ambayo serikali inaisimamia yenyewe lakini tuna kila sababu ya kuingia ubia katika miradi hii miwili kwa sababu bila kufanya hivyo ni sawa na kujipalia makaa wenyewe,alisema Muhongo.
Naye Meneja Miradi wa Tanesco, Simon Jilima alisema katika miradi hiyo, mradi wa Kinyerezi pekee umegharimu dola za Marekani milioni 183(zaidi ya Sh bilioni 200).
Tunatarajia kuanzia Juni 2014 hadi Oktoba mradi uwe umekamilika kwa vile zaidi ya megawatt 1500 zitazalishwa ambazo zikijumlisha na zile za awali zitafikia megewatt 3000.
Kituo cha Kinyerezi kitakuwa ni maalamu kwa uzalishaji umeme, Kipawa kudhibiti kiwango na ubora wa umeme, Gongolamboto kitatumika kutuliza nguvu ya umeme inayotoka Kinyerezi, alisema.
Chanzo: Mtanzania