unanitaka
JF-Expert Member
- Oct 7, 2014
- 2,178
- 1,045
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ameeleza kuwa Mameneja wa Shirika la umeme nchini (TANESCO) wanaosimamia Kanda mbalimbali nchini wataondolewa katika vyeo hivyo iwapo hawatatimiza maagizo mbalimbali waliyopangiwa na Wizara ya Nishati na Madini ifikapo Machi 1 mwaka huu.
Waziri wa Nishati na Madini alisema hayo wakati wa kikao chake na watendaji wa Shirika la Umeme nchini (TANESCO) na Taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara ya Nishati na Madini kilichofanyika katika Kituo cha kuzalishia umeme cha Mtera.
Profesa Muhongo alitaja maagizo hayo kuwa ni kuunganisha huduma kwa wateja wengi, kuwa na makusanyo makubwa ya bili za umeme, kupunguza manung’uniko ya wananchi katika huduma za umeme na uboreshaji wa mawasiliano kati ya Shirika hilo na wananchi.
“Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, ifikapo Machi Moja mwaka huu atatuthibitishia kama Mameneja hawa wataendelea na majukumu haya wanayoyasimamia ama la na hii itatokana na ufanisi wa utendaji katika majukumu tuliyowapangia,” alisema Profesa Muhongo.
Aidha, Waziri wa Nishati na Madini alisema kuwa Kitengo cha Uwekezaji cha Tanesco kama hakitakuwa na miradi mipya ya umeme ifikapo tarehe 2 Aprili mwaka huu, watendaji katika Ofisi hiyo wataondolewa katika nafasi hiyo kwa kushindwa kutimiza majukumu yake ipasavyo.
“Hapa hatuna mzaha kwani mahitaji ya umeme ni makubwa na tuna miradi mingi ya usambazaji umeme kwa wanannchi ikiwemo miradi ya REA na wananchi wanahitaji umeme kwa matumizi ya majumbani na kuanzisha viwanda vidogodogo, sasa bila miradi mipya ya umeme tutashindwa kusambaza umeme kwa wananchi hawa kwa kuwa kiasi cha umeme tulichokuwa nacho sasa bado hakitoshi,” alisema Profesa Muhongo.
Profesa Muhongo pia aliwaasa Mameneja wa TANESCO wa Kanda kuwakaribisha wawekezaji mbalimbali wa umeme ikiwemo miradi midogo ya uzalishaji umeme wa maji ili nchi iwe na umeme wa kutosha na sio kuwakatisha tamaa wawekezaji hao.
Vilevile Profesa Muhongo alisema kuwa watumishi watakaoleta urasimu katika kujadili masuala ya uwekezaji wa nishati wataachia ngazi kwani ndio wanaokwamisha juhudi za serikali katika kuongeza kiasi cha umeme nchini.
“TANESCO na EWURA kwa sasa pale anapojitokeza mwekezaji wa miradi ya umeme lazima mjadiliane naye kwa pamoja badala ya mwekezaji husika kwenda TANESCO baadaye anaenda EWURA au TPDC hivyo mwekezaji anapokuja jadilini naye kwa pamoja ili msitumie muda mrefu katika utekelezaji wa suala moja na hivyo kuchelewesha utekelezaji wa miradi mbalimbali,” alisema Profesa Muhongo.
Vilevile Profesa Muhongo aliwaagiza watendaji wa TANESCO katika vitengo vya ukaguzi kufanya kazi hiyo kwa ufanisi mkubwa ikiwemo usimamizi madhubuti wa nguzo za umeme ambazo baadhi huanguka kila inapofika msimu wa mvua na kusema kuwa suala hilo halikubaliki.