Simplicity.
JF-Expert Member
- Dec 19, 2013
- 2,636
- 1,661
Pamoja na kwamba ukimwi unaonekana kama vile ni ugonjwa wa kawaida, lakini, Ah wapi, ukimwi bado ni noma sana, ukiupata ndio utanielewa. Kuna jamaa zangu fulani walishawahi kunipigia simu kila mtu kwa wakati wake tofauti, kueleza masahibu ya ukimwi yalivyowapata. Ajabu ni kwamba walikuwa bado hawajawaeleza wenza. Niliwaambia acheni ujinga, waambieni wenza wenu kuwa mmeathirika ili kuwanusuru. Nimegundua kuwa wote wanaume kwa wanawake wana tabia ya kuwaficha wenzi wao pindi wanapokumbana na hilo janga. TAFADHALI ACHA KUISHI KWA MAZOEA, MCHUKUE MWENZI WAKO, AKIKATAA, TUMIA NGUVU ZA ZIADA MKAPIME ILI KUBAINI KAMA MNA MAAMBUKIZI AU LAH, MKIJIKUTA MNAO AU MMOJAWAPO ANAO, MTAJUA NAMNA YA KUISHI. Nawaambia baadhi yenu hamtaamini, matokeo, na kwa kweli kama utazingatia ujumbe wangu, nitakuwa nimekunusuru!
Ukimwi upo tena kwa kasi kubwa zaidi, hasa Dar.
Ukimwi upo tena kwa kasi kubwa zaidi, hasa Dar.